In Summary

• Stevo alikiri kwamba alishawahi kulala njaa mara tatu kabla mke wake hajaja lakini tangu waanze kuishi pamoja hawajawahi lala njaa kwani anajibiisha kama mwanamume.

Stevo akiri kupitia maisha magumu licha ya kuwa na jina kubwa.
Image: Instagram

Msanii kutoka Kibera Stevo Simple Boy amekiri madai ya mkewe kuwa ya kweli kwamba wanateseka sana na muda mwingi huwa wanalala bila kutia kitu chochote kinywani licha ya msanii huyo kuwa na jina kubwa lakini pia kuwa na menejimenti.

Katika mazungumzo na Vincent Mboya, Stevo alisema kuwa ni kweli yeye na mkewe Grace Atieno wanalazimika kulala njaa katika kile alisema kuwa hana riziki nyingine ya mbadala kando na muziki wake.

“Ni kweli, unajua kwa sababu unajua sina biashara tofauti na usanii, usanii ndio kazi yangu na kama hakuna shoo inabaki tunalala njaa. Hapo naunga mke wangu mkono,” Stevo alisema.

Wikendi, mke wake katika mahojiano ya kuliza alifichua kwamba msanii huyo licha ya kuwa ni jina kubwa, lakini bado anapitia maisha magumu sana.

Katika mahojiano hayo, Stevo alisema kuwa anahitaji msaada wa chakula na kutoa namba yake kwa yeyote mwenye moyo wa kusaidia kumpa msaada ili kumkwamua.

Haikubainika wazi kama madhira yake yanaweza kuhusishwa na kufeli kwa lebo ama ni kwa msanii huyo kutowekeza vizuri mapato ambayo aliyapata kutoka kwa kazi zake za Sanaa.

Stevo alikiri kwamba alishawahi kulala njaa mara tatu kabla mke wake hajaja lakini tangu waanze kuishi pamoja hawajawahi lala njaa kwani anajibiisha kama mwanamume.

View Comments