In Summary

• Mumewe Ruth Matete ambaye alikuwa na asili ya Nigeria alizikwa mwaka 2020 Julai na kuzikwa katika makaburi ya Lang’ata jijini Nairobi.

Bintiye Ruth Matete
Image: Instagram

Mchungaji na mwimbaji wa miziki ya injili humu nchini Ruth Matete alisalia na maswali mengi katika kichwa chake baada ya bintiye mfogo kumtambua marehemu babake katika picha.

Matete kupitia Instagram yake alipakia video ikimuonesha binti huyo mdogo akirukaruka baada ya kuoneshwa picha ya marehemu babake na moja kwa moja bila kusita mtoto huyo aliweza kumtambua kuwa ni baba yake – japo hajui kwamba ni marehemu kwa sasa.

Matete alipigwa na butwaa kwa mtoto huyo mdogo kumtambua babake nan a kusema kwamba tukio hilo lilimuacha na mmaswali mengi kuhusu vipi mtoto huyo akitaka kujua aliko babake huyo.

“Nimeshtuka sana! Sijawahi kumuonyesha picha hii. Sijawahi kuwa na mazungumzo naye kuhusu mada hii. Aliona picha akasema ni baba yake😢. Machozi yalinitoka tu. Sijui nilipata wapi ujasiri wa kuirekodi,” Matete alisema.

Alidokeza kwamba huenda atalazimika kwa kibarua cha kujibu maswali mengi kwani mtoto huyo kwa sasa anatizama filamu za watoto ambazo mara nyingi huonesha muunganiko wa familia – baba, mama na mtoto na huenda pia akaanza kuuliza aliko babake.

“Siku moja nitamwambia kuhusu hilo. Wakati anaweza kuelewa mambo. Lakini sasa nina wasiwasi. Anatazama katuni na anaona familia ni mama baba na dada na kaka. Je, akiniuliza sasa baba yuko wapi? Je, anaweza kuelewa? Nitamwambia nini?😢 Hawezi kuiacha picha hiyo tangu alipoiona.😭 Wakati huohuo, mtu huyu wa Kiyoruba alikuwa mkali sana. Chaaiii!!   💛” Matete alisema.

Mumewe Ruth Matete ambaye alikuwa na asili ya Nigeria alizikwa mwaka 2020 Julai na kuzikwa katika makaburi ya Lang’ata jijini Nairobi.

Mwanamume huyo alifariki mwezi Aprili mwaka huo lakini mwili wake ukasalia katika makafani ya KNH kwa miezi kadhaa kufuatia kisa cha moto kuteketeza nyumba walikokuwa wakiishi na kumuua – kisa ambacho kilichukuliwa kuwa cha utata na kwa wakati mmoja Matete mwenyewe kuhusishwa katika kile kilisemekana kwamba alipanga njama ya moto ili kumuuwa mumewe.

View Comments