In Summary

• Mamake Mohbad mnamo Jumanne, Novemba 21, 2023 anasema kwamba mwili wa mwimbaji huyo umetolewa kwa baba lakini amekataa uzikwe upya.

Mohbad na babake
Image: Screengrab

Baada ya miezi miwili ya mitazamo tofauti kuhusu kifo cha msanii Mohbad, hatimaye polisi wamekamilisha uchunguzi wa maiti iliyofukuliwa lakini inaarifwa kwamab babake Mohbad amekataa kuuchukua mwili huo kwa ajili ya kumpumzisha mwanawe.

Kwa mujibu wa blogu ya Linda Ikeji ambayo ilizungumza na polisi mmoja aliyetaka jina lake kubanwa, mzee huyo amearifiwa mapema wiki hii kuhusu kuuchukua mwili huo lakini amekataa kwamba hatoweza kuuchukua kwa ajili ya maziko kwa sababu kadhaa.

Mamake Mohbad mnamo Jumanne, Novemba 21, 2023 anasema kwamba mwili wa mwimbaji huyo umetolewa kwa baba lakini amekataa uzikwe upya.

Kwa mujibu wa polisi, baba mzazi ndiye pekee mwenye uwezo wa kukabidhiwa mwili huo pindi tu atakapotuma ombi la kukabidhiwa mwili, lakini mzee amekataa akisisitiza kwamba anataka uchunguzi mwingine wa DNA kufanywa ili kukubali kumzika mwanawe.

“Mwili uko katika chumba cha kuhifadhia maiti. Haijatolewa. Haingeachiliwa kwako na usingekuja na kuichukua. Hospitali haikuruhusu. Baba pekee ndiye anayeweza kuomba maiti hiyo kutolewa, ni baba tu na polisi wamesema siku yoyote akiomba angeipata mara moja. Tumewaambia muda wowote wakitaka waandike tu maombi lakini baba amekataa kufanya hivyo.”

“Kitaalam, ni baba ambaye anajizuia. Baba huyo amesema bado hatachukua hadi wafanye DNA na hilo ni tatizo lao la kifamilia. Babake akiandika [barua] leo, bila shaka maiti itatolewa na lazima aibebe maiti. Huwezi kuandika na kuiacha hapo. Kwa nani?”

Kumbuka kwamba mwimbaji huyo aliyeaga dunia Septemba 12, alizikwa siku iliyofuata, Septemba 13. Kufuatia utata wa kifo chake, uchunguzi wa maiti ulitakiwa na Wanigeria na mwili wake ukafukuliwa Septemba 21. Haujazikwa tena tangu wakati huo. na matokeo ya uchunguzi wa maiti bado hayajawekwa wazi.

Bw Aloba – babake - amesisitiza mara kwa mara kwamba lazima DNA ifanywe ili kujua asili ya kweli ya Liam, mtoto wa miezi saba wa marehemu Mohbad na mke wake, Wunmi.

View Comments