Watu 8 wafariki huku visa 137 vipya vya corona vikisajiliwa
- Visa 137 vipya vya corona na kufikisha jumla ya visa hivyo kuwa 39,586.
- Watu wanane wameaga dunia na kufikisha 743 watu ambao wameangamizwa na Covid 19
Kenya siku ya jumanne imesajili visa 137 vipya vya corona na kufikisha jumla ya visa hivyo kuwa 39,586.
Idadi hiyo ni kutoka sampuli 1,258 zilizopimwa katika saa 24 zilizopita na kufiklisha jumla ya sampuli zilizopimwa kuwa 566,536.
Katibu wa utawala wa wizara ya afya Rashid Aman amethibitisha kwamba wengi wa waliopatikana na ugonjwa huo ni wakenya .
Mgonjwa wa umri wa chini sana ana mwaka mmoja ilhali wa umri wa juu Zaidi ana miaka 81. Kati ya visa hivyo vipya 94 ni wanaume na 43 ni wanawake .
Aman amesema watu 296 wamepona na kuruhusiwa kwenda nyumbani na kufikisha idadi ya waliopona ugonjwa huo nchini kuwa 27,331.
Watu wanane hata hivyo wameaga dunia na kufikisha jumla ya idadi ya walioaga dunia kwa ajili ya corona kuwa 743
Nairobi inazidi kuongoza kwa visa vingi baada ya watu 64 kupatikana na virusi hivyo ikifuatwa na Turkana 34, Mombasa 12, Kiambu 8t, Trans Nzoia 4, Kericho, Kisii, Kisumu na meru kisa 1 kila moja