Watu 4 wafariki huku 22 wakipatikana na covid 19

Kenya   siku ya jumatatu imesajili visa 22 vya maambukizi ya ugonjwa wa corona  na kufikisha jumla ya idadio ya visa hivyo kuwa  564,78.

Idadi hiyo ni kutoka sampuli 595 zilizopimwa katika saa 24 zilziopita .

Visa vyote vipya ni vya wakenya  isipokuwa kisa kimoja .

Watu 376 wamepona na kufikisha idadi ya waliopona ugonjwa huo kuwa 27,035

Katibu wa utawala wa wizaa ya Afya  Rashid Aman  amesema wafanyikazi 129 wa fya wameambukizwa ugonjwa huo .Hata hivyo Kenya leo imewapotea watu wane kwa ugonjwa huo na kufikisha idadi ya walioaga dunia kuwa  735.