Shule kufunguliwa jumatatu ijayo ,Magoha atangaza

Muhtasari

 

  •  Shule kufunguliwa Jumatatu tarehe 12 mwezi Oktoba
  • Shule zote zilifungwa mwezi machi tangu kuanza janga la corona lilipotangazwa nchini 
  • Awali serikali iliwataka walimu kuripoti shuleni kwa matayarisho ya kufunguliwa kwa shule
  • Wanafunzi wa vyuo vikuu tayari wamerejea shuleni 

 

Waziri wa Elimu George Magoha
Waziri wa Elimu George Magoha

 

Shule kote  nchini zitafunguliwa jumatatu tarehe 12 mwezi huu .

 Wanafunzi  wa gredi ya nne  ,darasa la nane na watahiniwa wa kidato cha nne  wanatarajiwa kuripoti shuleni siku hiyo .

 
 

 Magoha amesema mtihani wa KCPE  utaanza machi tarehe 22 mwaka ujao na kumalizika machi tarehe 24 mwka wa 2021

Mtihani wa KCSE utaanza machi tarehe 25 mwaka wa 2021 na kukamilika  Aprili tarehe 16 mwaka wa 2021

Kupitia taarifa Magoha amesema wanafunzi wote watakaripoti shuleni watatakiwa kuvalia maski  pamoja na  walimu na mtu yeyote anayekwenda shuleni .Wizara ya elimu imetaka usafi kudumishwa na pawepo vifaa vya kuhakikisha wanafunzi wananawa mikono na kutumia sanitaza

Kalenda ya shule mwaka huu
Image: MOE

 Wizara hiyo imesema ingawaje kuwatenganisha wanafunzi wakiwa darasani itakuwa changamoto ili kuzuia mrundiko ,hilo halifai kutumiwa kama kigezo cha kuwazuia wanafunzi kundelea na masomo yao .Shule ambazo zilikuwa zikitumiwa kama  vituo vya karantini zimefukizwa na kuwa tayari kwa wanafunzi kuzitumia ilhali zile zilirataibiwa kutumiwa kama karantini na hazikutumiwa zitafukizwa dawa kwanza .Wanafunzi wa baadhi ya vyuo vikuu tayari wamerejea shuleni .Wazazi awali walitayarajia kwamba shule zingefunguliwa mwaka ujao kama ilivyokuwa imetangaza wizara ya Elimu lakini baada ya kupungua kwa maambukizi ya corona ,imeamua kuzifungua shule mwaka huu .

Wazazi waanza kujiandaa kwa shule kufunguliwa

Wazazi waanza kujiandaa kwa shule kufunguliwa

By Davis Ojiambo

Je Wazazi wako tayari kuwaachilia wanao kurudi shuleni?+Podi ya Yusuf Juma

Je Wazazi wako tayari kuwaachilia wanao kurudi shuleni?+Podi ya Yusuf Juma

By Yusuf Juma

Magoha awataka walimu kutayarisha shule kufunguliwa

Magoha awataka walimu kutayarisha shule kufunguliwa

By Davis Ojiambo

 Katika mwongozo wa kufungua shule ,wizara ya elimu imesema shule zote zimeunganishwa karibu na vituo vilivyo karibu vya afya kabla ya kufunguliwa .walimu wametakiwa kuendelea kuwapa watoto usaidizi wa kisaikolojia wakati wa janga la corona .bodi za usimamizi wa shule na walimu wakuu wamepewa jukumu la kuhakikisha kwamba kanuni hizo zinatekelezwa