Magoha ameyasema hayo jumatatu katika mkutano na wadau wa sekta ya elimu ili kujadili mwongozo wa kuzifungua shule katika tasasisi ya ustawishaji wa Mtaala.
Mwezi julai wizara ya elimu ilitangaza kwamba shule zitafunguliwa januri mwaka ujao . Magoha hata hivyo alisema uamuzi huo unaweza kubadilishwa .
Katika wiki moja iliyopita kumekuwa na shinikizo kwamba shule zifunguliwe huku wamiliki wa shule za kibinafsi wakiitaka serikali kuzingatia uamuzi wa kutaka kuzifungua shule mwaka ujao .
Kupungua kwa visa vya maambukizi ya corona pia kumechangia wito huo wa kufunguliwa kwa shule . Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kutoa mwongozo mpya mwishoni mwa mwezi huu huku akilenga kufungua sekta za uchumi ambao umevurufika tangu mwezi machi .
Shule za kibinafsi na walimu wakuu wanaitaka serikali kufungua shule mwezi ujao ili watahiniwa wa mwaka waweze kuifnya mitihani yao . Januari ilikuwa imetangazwa kama tarehe ya kufunguliwa kwa shule iwapo visa vya corona vingezidi lakini hali hiyo sasa imebadilika huku jumla ya visa 150 vikiripotiwa kila siku .
Hata hivyo muungano wa walimu KNUT umekosoa mpango wa kuzifungua shule mapema kabla ya januari .katibu mkuu Wilson Sossion amesema shule haziko tayari kufunguliwa hata kwa watahiniwa pekee .