Magoha awataka walimu kutayarisha shule kufunguliwa

Waziri wa elimu George Magoha amewataka walimu wakuu kuhakisha kuwa shule ziko katika hali nzuri tayari kukaribisha wanafunzi shule zinapatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni.

Magoha alisema kwamba shule zitafunguliwa hivi karibuni na ni muhimu wanafunzi wapate zikiwa katika hali nzuri ili wandelee na masono bila tatizo lolote.

Serikali kupitia agizo la rais Uhuru Kenyatta ilifunga shule mwezi Machi mwaka huu kutokana na janga la Covid-19.

Tangu kufungwa kwa shule mwezi machi, shule nyingi zimemea nyasi huku zikisalia mahame na zingine majengo yameharibika.

“Wacha walimu wafanye kadri ya uwezo wao kufanya shule ziwe na mazingira mazuri ya kusomea. Watoto watarejea shuleni hivi karibuni,” Magoha alisema.

Soma habari zaidi hapa;