In Summary

 

  •  Othuol amekuwa akiugua tangu mwaka jana 
  •   Mchekeshaji huyo  alikuwa Miongoni mwa walionufaika na shilingi elfu 10  za kuwasaidia wasanii wakati wa corona 
  • Churchil,wenzake katika fani na wakenya wametumia mitandao ya kijamii kumuomboleza 

 

Othuol Othuol

 Mchekeshaji  wa Churchill show  Ben Morris anayefahamika kwa jina lake la usanii Othuol Othuol ameaga dunia .

 Staa huyo wa jukwaa la vituko aliaga dunia katika hospitali ya KNH ambako amekuwa akipokea matibabu baada ya kupatikana na uvimbe katika ubongo wake

  Mwanzilishi wa kipindi hicho  Danile Ndambuki amethibitisha kifo cha Othuol akiandika katika mitandao ya kijamii ;

 

 ‘Maisha ni mafupi .Mungu hutoa na mungu huchukua .Sote tuko safari . Lala salama Othuol’

 Othuol amekuwa nje na ndani ya hospitali kwa muda  .Wiki chache zilizopita alikimbizwa hospitalini huku marafiki na jamaa zake wakiwataka wakenya kumuombea . Wakenya wengi wamefurika mitandao ya kijamii kumuomboleza Othuol .

 

View Comments