In Summary

 

  • Moderna imepokrea zaidi ya  dola bilioni 1 za kufanya utafiti kutoka kwa serikali ya  Marekani  na ina mkataba wa  dola bilioni1.5 kutoa dozi milioni 100 za  chanjo yake
  •  Kampuni hiyo sasa imesema itatafuta idhini ili kuruhusiwa  kutumia chanjo hiyo  kupambana na virusi vya corona 

 

  Kampuni ya kutengeza dawa ya Moderna Inc  imesema jumatatu kwamba chanjo yake dhidi ya corona ina uwezo wa asilimia  94.5% kuzuia virusi vya corona  na kuwa kampuni ya pili ya Marekani katika kipindi cha wiki moja  kutoa matokeo  yanayozidi matarajio

 Kampuni hiyo sasa imesema itatafuta idhini ili kuruhusiwa  kutumia chanjo hiyo  kupambana na virusi vya corona 

 Tathmini ya kwanza ya matumizi ya chanjo hiyo imetokana na  na visa 95 vya corona

 Matokeo hayo yametolewa wiki moja baada ya kampuni ya  Pfizer Inc  na mshirika wake wa ujerumani  BioNTech SE  kusema kwamba chanjo yao ilikuwa na uwezo wa  Zaidi ya asilimia 90 kuzuia corona .

Moderna,  ambayo ilianza kutambulika mwaka wa 2018 imepokrea zaidi ya  dola bilioni 1 za kufanya utafiti kutoka kwa serikali ya  Marekani  na ina mkataba wa  dola bilioni1.5 kutoa dozi milioni 100 za  chanjo yake . Serikali ya Marekani ina chaguo la kuitisha dozi nyingine milioni 400 na Moderna pia ina mikataba nan chi nyingine kutoa chanjo hiyo

 

View Comments