Last Updated On 19 November 2020 1 Min Read
Tanzia
Mwakilishi wa kaunti ya Nakuru afariki Corona
Samwele Karanja alikuwa mwakilishi wa wadi ya London
In Summary
- Ni kiongozi wa pili kuaga dunia kwa ajili ya corona katika bunge hilo
- Alikuwa akiwakilisha wadi ya London
Bunge la kaunti ya nakuru limekumbwa tena na msiba baada ya kuaga dunia kwa mwakilishi mwigine wa kaunti kwa ajili ya corona .
Gavana wa kaunti hiyo Lee Kinyanjui amethibitisha kifo cha mwakilishi wa wadi ya London Samwel Karanja siku ya alhamisi . Kifo cha Karanja kinmetokea wiki mbili tu baada ya mwakilishi wa Hell’s Gate John Njungna
Katika risala zake za rambi rambi kwa familia ya Karanja gavana huyo amesema bunge la kaunti sasa linaomboleza kifo cha mwakilishi wa tatu baada ya mwingine kuaga dunia mwaka jana .
Gavana Lee amesema mwakilishi huyo alikuwa na jukumu kubwa la kuwakilisha eneo lenye jamii nyingi .
" Alikuwa mtu mkweli na mwenye bidii .uwezo wake kusuluhisha matatizo utakoswa sana’ Gavana