In Summary

  • Thugge amekubali kutoa ushahidi dhidi   uhuruto 

Aliyekuwa waziri wa fedha Henry Rotich ambaye alitimuliwa kutokana na  madai ya ufisadi sasa yuko mashakani baada ya aliyekuwa katibu wake wa kudumu Kamau Thugge kukubali kutoa ushaidi dhidi yake.

Mkurugenzi wa mashtaka ya umma Nooordin Haji anaamini kwamba Thugge ambaye alikuwa ameshtakiwa pamoja na Rotich atamsaidia katika kesi dhidi ya Rotich.

Thugge na Koech walikuwa miongoni mwa watu 20 waliyoshtumiwa kwa  kushiriki ufisadi kuhusiana na ujenzi wa mabwaya ya Arror na Kimwarer wakishirikiana na makurugenzi wa kampuni ya CMC di Ravenna ya Italia.

Lakini Thugge ambaye alihudumu chini ya Rotich, aliafikia makubaliano na kiongozi wa mashtaka ya serikali na huenda akasimama kizimbani kutoa ushahidi ya Rotich.

Wakili anayefahamu kesi hiyo aliambia meza yetu ya habari kwamba hatua ya kumgeuze Thugge kuwa shahidi kumepiga jeki kesi dhidi ya Rotich.

Rotich anakabiliwa na kesi kuhusiana na sakata inayokisiwa kuwa ya shilingi bilioni 64.

"DPP alihitaji mtu mashuhuri wa ndani kutoa ushahidi. Baada ya kushtaki maafisa wengi, hakukuwa na mtu wa kutoa ushahidi dhidi ya wale walioshtakiwa. Kwa hivyo ni jambo la busara kupata makubaliano na Thugge," wakili huyo alisema.

Haji pia amezungumza juu ya kujadiliana na Katibu Mkuu wa zamani wa Wanyamapori Susan Koech ili atoe ushahidi dhidi ya Rotich. Kwa hivyo, serikali inaweza kuondoa mashtaka yanayomkabili Thugge na Koech wakati upande wa mashtaka unapoenda kumsulubu Rotich.

View Comments