Moto
Bunge la Garissa lateketea katika mkasa wa moto wa asubuhi
Karani wa bunge hilo Mohamed Santur ametaja hasara iliyosababisha na mkasa huo wa moto kama ‘Kubwa’
- “ Nilipofika nilimpata mlinzi mmoja akijaribu kuuzima moto huo .Nilimsaidia lakini tulizidiwa na kiasi cha moto uliokuwa ukiwaka’ amesema Abdi .
- Joseph Wambua, mhudumu wa boda boda alijutia kwamba wazima moto wlaichukua muda mrefu-takriban dakika 45 kujibu tukio hilo na kufanya moto huo kusambaa kwa afisi zilizo karibu
Bunge la kaunti ya Garissa na afisi zilizo karibu zimeteketea mapema leo katika kisa cha moto ambao chanzo chake hakijajulikana .
Tukio hilo mwendo wa saa mbili na dakika 20 kilitokea wakati mto ulipozuka katika bunge la kaunti na kusambaa hadi katika afisi zilzio karibu . Ilichukua dakika 45 kwa zima moto wa Garissa kufika eneo la mkasa licha ya kuwa umbali wa kilomita 5 kutoka majengo ya bunge hilo .
Juhudi za wananchi kujaribu kuuzima moto huo ziliambulia patupu kwa sababu sakafu ya jengo hilo imewambwa kwa vitambaa vya nguo na dari ni la mbao zilizopigwa rangi .
Waokoaji pia walifaulu kuliondoa gari ambao lilikuwa kkaribu na jengo hilo ili kulipeusha na hasara ya kuchomeka . Mohamed Abdi mlinzi katika duka zilizo karibu amesema aliona moshi mweusi ukitokea katika jengo la bunge na kisha akakimbia kutazama kilichokuwa kikifanyika .
“ Nilipofika nilimpata mlinzi mmoja akijaribu kuuzima moto huo .Nilimsaidia lakini tulizidiwa na kiasi cha moto uliokuwa ukiwaka’ amesema Abdi .
Joseph Wambua, mhudumu wa boda boda alijutia kwamba wazima moto wlaichukua muda mrefu-takriban dakika 45 kujibu tukio hilo na kufanya moto huo kusambaa kwa afisi zilizo karibu
Karani wa bunge hilo Mohamed Santur ametaja hasara iliyosababisha na mkasa huo wa moto kama ‘Kubwa’