In Summary
  • Mkuu wa DCI George Kinoti amesema Kipkogei alipatikana katika maficho yake  Ray Farm   Uasin Gishu  siku ya jumamosi alasiri
  • Kipkogei  na  ndugu yake mwingine ambaye hajakamatwa walimshambulia kaka yao mdogo na kumuua kwa sababu ya utata kuhusu umiliki wa shamba

Mwanamme ambaye amekuwa mafichoni kwa kushukiwa kumuua kakake kwa sababu ya  mzozo kuhusu umiliki wa shamba amekamatwa .

 Alex Kipkogei, 37,  anashtumiwa kwa kumuua kakake mdogo  baada ya mzozo huko huko  Chesitek-Keiyo North. 

Mkuu wa DCI George Kinoti amesema Kipkogei alipatikana katika maficho yake  Ray Farm   Uasin Gishu  siku ya jumamosi alasiri

Kipkogei  na  ndugu yake mwingine ambaye hajakamatwa walimshambulia kaka yao mdogo na kumuua kwa sababu ya utata kuhusu umiliki wa shamba . Mshukiwa atafikishwa kortini  siku ya jumatatu huku polisi wakiendelea kumsaka mshukiwa wa pili aliyetajwa kama  John Lotema.

" Iwapo una Habari zitakazopelekea kukamatwa kwake tafadhali piga simu kwa nambari isiokuwa na tozo  0800 722 203," Kinoti  amesema

 

View Comments