In Summary

•Steve Olumbe alikamatwa karibu na kituo cha mabasi cha Homabay alipokuwa anatembea huku akiwa amebeba shoka na panga zenye damu.

•Baada ya kuangamiza nyanyake Olumbe aliendelea kuua ng'ombe watatu pamoja na na mbuzi watano.

Wakaazi katika eneo ambalo mshukiwa Steve Olumbe alimuua nyanyake na wanyama wanane huko Homa Bay.
Image: ROBERT OMOLLO

Polisi katika kaunti ya Homabay wanazuilia jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 24 ambaye aliua nyanya yake pamoja na mifugo wanane nyumbani kwao katika kijiji cha Ruga, eneo bunge la Homabay Town.

Steve Olumbe alikamatwa karibu na kituo cha mabasi cha Homabay alipokuwa anatembea huku akiwa amebeba shoka na panga zenye damu.

Mshukiwa anaripotowa kutekeleza unyama huo mwendo wa saa nane usiku wa kuamkia Jumanne wakati nyanya yake Priscilla Were (70) alikuwa amelala.

Baada ya kuangamiza nyanyake Olumbe aliendelea kuua ng'ombe watatu pamoja na na mbuzi watano.

Bado haijabainika kilichompelekea mshukiwa kutenda kitendo kile ila wanakijiji wamedai ana matatizo ya kiakili.

Wakaazi katika eneo ambalo mshukiwa Steve Olumbe alimuua nyanyake na wanyama wanane huko Homa Bay.
Image: ROBERT OMOLLO

Mmoja wa wajomba wake, Silas Ngare aliambia wanahabari kwamba jamaa yule alitumia madawa kuthibiti hasira yake.

"“Mshukiwa na marehemu walikuwa wakilala nyumba moja pamoja na mwanafunzi wa darasa la saba ambaye wana uhusiano wa karibu. Alikuwa na nia ya kumuua mtoto huyo pia kabla ya kutoroka,” Ngare alisema

Kamanda wa polisi katika kaunti ya Homabay Esther Seroney amesema walinzi walipiga ripoti kuhusu tukio hilo kabla ya mshukiwa kutiwa mbaroni.

"Walimwona mwanamume huyo saa nne asubuhi kabla ya kuripoti kwa Chifu wa eneo Bob Lango. Tulimkamata mshukiwa katika kituo cha mabasi,” Seroney alisema

Walinzi walisaidia maafisa wa polisi kukamata mshukiwa na kumuweka kizuizini.

Mwili wa marehemu ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya Homa Bay hukumshukiwa akisubiri kupelekwa hospitalini kufanyiwa ukaguzi wa kiakili kabla ya kushtakiwa kwa mauaji..

View Comments