In Summary

•Mapema saa moja asubuhi watu wanaanza kukusanyika kwenye Visiagi na baada ya nusu saa msongamano mkubwa wa watu unashuhudiwa wakisubiri zamu yao.

Wapekhulu kwenye Kisiagi
Image: HANDOUT

Biashara ya Visiagi huko maeneo ya Kawangware vimeongeza umaarufu wake katika eneo hilo.

Visiagi katika eneo hilo vimeleta nafasi za kazi na vyakula vya bei nafuu.

“Tuna bahati kwamba tuna maeneo mingi  ya kusiaga mahindi, hatuwezi kulala njaa kwa sababu bei ya unga wa mahindi ya Kisiagi ni ya bei ya chini sana. Siwezi kununua unga wa mahindi ya Duka, naona haina ladha, hainiridhishi hata kidogo na bei yake  ni  ghali”David Macharia alisema.

Katika kilele cha mzozo wa kisiasa mali nyingi hua zinateketezwa lakini wakati huo hakuna yule ambaye anasongea Kisiagi kwa madhumuni ya kuiharibu.

Wanadai kuwa kuharibu Kisiagi inawezasababisha njaa kitu ambacho wenyeji hawajazoea hata kidogo.

Kisiagi kizuri  kinaweza gharimu kati ya sh.120, 000 na sh.140, 000.

Wakaazi wanasema wanapendelea unga wa mahindi ya Kisiagi kuliko mahindi ya Duka kwa sababu ya uwezo wake wa kumudu kwa tumbo.

Maeneo hayo  ina idadi kubwa ya watu kutoka magharibi na Luo nyanza, watu hao wanapenda ugali kama mlo kushinda vyakula vingine.

”Visiagi ni vingi kwa sababu Wakisii,Waluhya na Wajaluo ndio wakaazi wakuu wa Kawangware. Kwa asili tunapenda Ugali. Nisipokula ugali hata kutembea inakuwa shida, hivyo naishia kurudia kula Ugali na vitoweo tofauti”, alisema Omariba.

Mapema saa moja asubuhi watu wanaanza kukusanyika kwenye Visiagi na baada ya nusu saa msongamano mkubwa wa watu unashuhudiwa wakisubiri zamu yao.

View Comments