In Summary

•Mabao kutoka kwa Jamal Musiala na Ilkay Gundogan yalitosha kuipa changamoto kikosi chake Marco Rossi, ingawa mechi hiyo haikuwa rahisi kwa wenyeji kama ilivyotarajiwa.

•Ujerumani sasa imefuzu nao Hungaria bado wana nafasi ya kusonga mbele kwa hatua ya 16 bora, ikiwa wataweza kushinda dhidi ya Scotland katika mechi yao ya mwisho ya kundi A.

Ikay Gundogan na Jamal Musiala washerehekea baada ya kufunga bao

Ujerumani imefuzu kwa hatua ya 16 bora katika Euro 2024 baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Hungaria huko Stuttgart mnamo jana.

Ujerumani ilijua ushindi huo ungeifanya kuwa timu ya kwanza kusonga mbele katika hatua za mwisho za mashindano hayo ya makundi, nacho kikosi chake Julian Nagelsmann hakikukosea matarajio hayo.

Mabao kutoka kwa Jamal Musiala na Ilkay Gundogan yalitosha kuipa changamoto kikosi chake Marco Rossi, ingawa mechi hiyo haikuwa rahisi kwa wenyeji kama ilivyotarajiwa.

Bao la kwanza la Ujerumani lilitokea baada ya mlinda mlango wa Hungaria, Peter Gulacsi, kudaka shuti la Gundogan lakini akashindwa kuidhibiti vizuri, na badala yake akalirudisha kwa Gundogan ambaye alimpa pasi Musiala, na mchezaji huyo mahiri wa Bayern Munich akafunga kwa urahisi bila ya ugumu wowote.

Hungaria hata hivyo haikuogopa bao la Ujerumani la kwanza, na walikuwa na fursa murua ya  kusawazisha wakati mkwaju wa kichwa wa Bernabas Varga ulipopita juu ya lango na kumpa Manuel Neur wakati mgumu.

Ujerumani, baadaye, iliongeza bao la pili kupitia kombora lake Gundogan, ambalo lilizima matumaini ya Hungaria.

Ujerumani sasa imefuzu nao Hungaria bado wana nafasi ya kusonga mbele kwa hatua ya 16 bora, ikiwa wataweza kushinda dhidi ya Scotland katika mechi yao ya mwisho ya kundi A.

View Comments