Seneta wa Kakamega Boni Khalwale amempongeza mgombeaji wa kiti cha ugavana wa ODM Fernandes Barasa baada ya kushinda kiti cha ugavana wa Kakamega.
Khalwale kwenye tweet alisherehekea gavana mteule na kumpongeza Cleophas Malala wa ANC kwa kupigana vilivyo.
"Hongera Barasa Fernandes kwa ushindi wako na Cleophas Malala kwa pambano lako la moyo," Khalwale aliandika.
Barasa alipata kura 192,929 dhidi ya Malala aliyepata kura 159,508.
Alishinda katika majimbo yote ya kanda ya kusini na mengine mawili ya kanda ya kaskazini.
ODM sasa imeshinda viti tisa kati ya 12 vya ubunge na 48 kati ya viti 60 vya MCA huko Kakamega.