(+Video)Nililia mwaka wa 2007, baada ya baba yangu kushindwa katika uchaguzi mkuu-Winnie Odinga
- Winnie Odinga asema alilia mwaka wa 2007 baada ya baba yake kuoteza uchaguzi mkuu
- Pia alisema miaka hiyo nyingine ambayo baba yake amekuwa akipoteza uchaguzi mkuu hajalia
- Winnie alisema sisasa iko katika damu,na kuwa ni jambo la furaha sana kufanya kazi na baba yake
KInara wa chama cha ODM Raila Amollo Odinga amewania kiti cha urais mara nne bila ya kufaulu.
Mwanawe Winnie Odinga akiwa kwenye mahojiano na radiojambo aliweka wazi kwamba kuna wakati walilia kama familia baada ya baba yake kupoteza uchaguzi huo.
"Mwaka wa 2007 wakati wa uchaguzi mkuu, wakati baba yangu alipotezza uchaguzi mkuu wa urasi, 2007 ni lilia
Mwaka wa 2017, baada ya Raila kupoteza uchaguzi mkuu, aliapishwa katika bustani ya Uhuru wakati huo kila mtu mwenye alikuwa katika hafla hiyo alikuwa ameweka maisha yake hatarini
Nilimsaidia baba yangu kama vile huwa nasaidia familia yangu na wala si siasa, siasa iko kwa damu yangu," Alieleza Winnie.
Wakati wa hafla hiyo Winnie alifichua kwamba babayake, Raila hakutaka ahudhurie hafla hiyo bali alimwambia lazima awe naye.
"Baba yabgu hakutaka niende katika hafla hiyo, unakumbuka vile aliyekuwa rais wa marekani Kennedy vile alipigwa risasi na mke wake akamshika, niliambia baba yangu kuwa nitakuwa hapo kitendo hicho kikitokea,"
Winnie aliweka wazi kwamba ni jambo la kupendeza kufanya kazi na baba yake.
Hii hapa video ya mahojiano hayo;
The video could not be loaded.