In Summary
  • Mke wangu aliniacha baada ya kumwambia twende tukaishi mashambani
  • Kila siku ya juma katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha patanisho, wengi wamekuwa wakipatanishwa baada ya kukosana

Kila siku ya juma katika kipindi cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha patanisho, wengi wamekuwa wakipatanishwa baada ya kukosana.

Siku ya Ijumaa bwana KInyua alituma ujumbe ili apanishwa na mkewe ambaye wamekuwa pamoja kwa zaidi ya miaka mitano, na walikosana miaka 6 iliyopita.

"Naomba mnipatanishe na mke wangu wa zaidi ya miaka 5. Tulikosana miaka 6 iliyopita. Tulikuwa tunaishi Nairobi na nikaamua twende nyumbani baada ya kazi yangu kuisha akakataa. Nikaenda na akaniletea mtoto baadaye

 nataka kumuomba msamaha kama nimemkosea, nataka tulee mtoto pamoja aliniachia mtoto ambaye nimekuwa nikimlea," Inyua Alisema.

Baada ya kufanya juhudi za umfikia mkewe alikuwa na haya ya kusema,

"Haiwezekani nishaaendelea na maisha yangu,"Mama Jim alisema.

 

 

 

View Comments