In Summary
  • Mkikosana haya basi walete kwenye kitengo cha patanisho ili wapanishwe na kurudisha uhusiano wao
  • Katika kitengo cha patanisho, bwana Gabriel alituma ujumbe ili apanishwe na mke wake ambaye wamekuwa pamoja kwa miaka 9 baada ya kutoroshwa nyumbani na mjomba wake
Ghost na Gidi
Image: Studio

Mkikosana haya basi walete kwenye kitengo cha patanisho ili wapanishwe na kurudisha uhusiano wao.

Katika kitengo cha patanisho, bwana Gabriel alituma ujumbe ili apanishwe na mke wake ambaye wamekuwa pamoja kwa miaka 9 baada ya kutoroshwa nyumbani na mjomba wake.

"Naomba mnipatanishe na mke wangu wa miaka 9. Nilirudi nyumbani nikapata mjomba wake amemtorosha na watoto eti anaenda kumtafutia kazi Nairobi na nimewazoea. Mwanzo walimpeleka Voi, kufika huko nikapata wamempeleka Nairobi..."Alieleza Gabriel.

Baada ya kufanya juhudi za kumfikia mkewe alikuwa na haya ya kusema;

"Huyu mwanamume aliniwekea chakula sumu, nillijua kuwa kina sumu baada ya kubadili rangi na kuwa cheusi

Akiwa na pesa ni mbaya sana lakini akiwa hana pesa anakuwa yuko sawa,akitaka turudiane aende kwa wazazi wangu

Amekuwa akienda kwa mganga ili anitoe kafara, muhubiri wetu aliniambia hayo na anapenda wanawake kuna wakati alinizamba kofi kwa ajili ya mwanamke,"

Haya ni madai ambayo Gabriel aliyakana.Kwa mengi zaidi tembelea Radiojambo Youtube.

 

 

 

 

 

View Comments