logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Embarambamba taabani baada ya kurekodiwa akishiriki densi chafu na mashabiki

Video inayoonyesha Embarambamba kwenye klabu akiwa amelaza mwanadada chini na kuchezea densi juu yake inazunguka mitandaoni

image
na Samuel Maina

Burudani25 May 2021 - 03:49

Muhtasari


  • • Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya uainishaji wa Filamu nchini Kenya (KFCB Ezekiel Mutua amesema tendo hilo ni la aibu na kuwa Embarambamba amevuka mipaka
  • •Video zinazoonyesha Embarambamba kwenye klabu akishiriki densi zisizo na maadili zinazunguka mitandaoni
Embarambamba

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Christopher Nyangwara almaarufu kama Embarambamba amekashifiwa sana baada ya video zinazomuonyesha mwanamuziki huyo akicheza densi za aibu kusambazwa mtandaoni.

Kwenye video hizo, Embarambamba alionekana kujiachilia kwenye klabu na kucheza na wanadada kwa mitindo isiyo ya Kikristo.

Video moja haswa iliyomuonyesha msanii huyo akiwa amemlaza mwanadada chini na kuchezea juu yake ilikashifiwa sana huku wanamitandao wengi wakisema kuwa mwanamuziki huyo kweli amepotea njia sasa.

Kati ya walioonyesha kutoridhishwa kwao na video hizo ni pamoja na Mkurugenzi mtendaji wa bodi ya uainishaji wa Filamu nchini Kenya(KFCB), Ezekiel Mutua ambaye alisema kuwa kitendo hicho ni cha aibu sana.

"Embarambamba.. hiyo ni aibu. Umepita mipaka sasa!" Mutua aliandika.

 

Mtangazaji wa habari za NTV, Lofty Matambo pia ameeleza masikitiko yake baada ya kuziona video zile.

"Nimesikitishwa sana na Embarambamba kama mmoja wa waliomshika mkono na hata kumhoji kwenye televisheni ya kitaifa. Video inayozunguka haikaribiani kabisa na anachojifanya kuwa, ati mwanamuziki wa nyimbo za injili" Matambo aliandika.

Video ingine inayomuonyesha Embarambamba ameinua shabiki mmoja juu na kumuekelea kwa kiuno chake kisha kucheza densi naye pia imeibua gumzo sana mtandaoni.

Baadhi ya Wakenya walisema kuwa huo ndio ulikuwa mwanzo wa kuanguka kwa mwanamuziki huyo aliyepata umaarufu mkubwa kutoka na sarakasi anazofanya kwenye nyimbo zake.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved