logo

NOW ON AIR

Listen in Live

"Alinifanya kama mtoto" Fayvanny afichua vitu ambavyo anapeza zaidi kwa aliyekuwa mpenzi wake, Rayvanny

Ingawa Fayvanny amesema wazi kwamba hamtamani tena mwanamuziki huyo kama mume wake, amekiri kwamba kuna mambo kadhaa kumhusu ambavyo anapeza sana.

image
na Radio Jambo

Burudani24 October 2021 - 09:27

Muhtasari


•Mama huyo wa mtoto mmoja amefichua kwamba Rayvanny alikuwa anamdekeza sana haswa alipokuwa mjamzito, jambo ambalo lilimfanya ajihisi kama mtoto.

•Alikiri kwamba moyo wake ulivunjika na alilia sana wakati Rayvanny alitambulisha mpenzi wake wa sasa Paula Kajala siku ya Valentines mwaka huu  kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Aliyekuwa mpenzi wa  Rayvanny, mfanyibiashara Fahyma almaarufu kama Fayvanny amefunguka kuhusu mahusiano yao yalivyokuwa kabla ya ndoa yao kuvunjika miaka michache iliyopita.

Alipokuwa kwenye mahojiano katika Wasafi Media hivi karibuni, Fayvanny alithibitisha wazi kwamba kwa sasa hana mahusiano yoyote ya kimapenzi na Rayvanny ila wao ni marafiki wakubwa sana.

Ingawa Fayvanny amesema wazi kwamba hamtamani tena mwanamuziki huyo kama mume wake, amekiri kwamba kuna mambo kadhaa kumhusu ambavyo anapeza sana.

"Simpezi kama mume wangu. Si mtu mbaya, ni mzuri. Ana vitu vingi vizuri . Mabaya huwa machache sana lakini wengi wetu tukifanyiwa baya moja ndio tunasahau mema yote. Nakumbuka itu vingi kumhusu" Fayvanny alisema.

Mama huyo wa mtoto mmoja amefichua kwamba Rayvanny alikuwa anamdekeza sana haswa alipokuwa mjamzito, jambo ambalo lilimfanya ajihisi kama mtoto.

Fayvanny alieleza kwamba mwanamuziki huyo hakumtaka afanye kazi zozote za nyumbani ila alitaka azifanye yeye mwenyewe ama asaidiwe na yaya.

"Kipindi ambacho nilikuwa mjamzito alikuwa ananifanya kama mtoto. Alikuwa ananidekeza sana. Alitaka afanye kila kitu yeye, hakutaka ata niiname ama nishike fagio. Kulikuwa kuna dada ambaye alikuwa anapika.. Rayvanny anajua kupika pia, mara nyingi alikuwa ananikaangia viazi. Hakutaka nile vya barabarani" Fayvanny alieleza.

Alikiri kwamba moyo wake ulivunjika na alilia sana wakati Rayvanny alitambulisha mpenzi wake wa sasa Paula Kajala siku ya Valentines mwaka huu  kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

"Nilisema asante Mungu, ijapokuwa iliniuma sana lakini nikaona sina sababu ya kuumia. Nilisema asante Mungu  wewe ndio ulimleta na ukamchukua. Nililia sitakuwa muongo. Niliumia sana" Alikiri Fayvanny.

Fayvanny alisema  kwamba kwa sasa hana mahusiano na mwanaume yeyote huku akidai kuwa hako tayari kujitosa kwenye mahusiano mengine.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved