Video moja imezua tafrani katika mitandao ya kijamii ikionyesha wakati mchungaji alipozuka katika barabara moja akiendesha gari lake la kifahari.
Katika video hiyo, pindi tu mchungaji huyo alipozuka katika barabara ya mtaa wa karibu na kanisa lake, makumi ya watu wanaoaminika kuwa waumini wa kanisa lake walifurika kando ya barabara, kila mmoja aking’ang’ana kugusa gari ili kupata Baraka.
Mchungaji alikuwa akiliendesha gari lake la kifahari kwa mwendo wa kobe huku kando kando likizungukwa na mabaunsa ambao walikuwa wanajaribu kuwathibiti waumini waliokuwa na kiu kubwa ya kuligusa gari ili kupata Baraka.
Hata hivyo, video hiyo imezua hisia tofauti kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.
@ studio ya inkredible “Walimpenda… hicho ndicho kitu pekee ninachokiona hapa!!! Inaitwa upendo wa kweli.. Sahau kila jambo lingine,” @excelhairlab “Ikiwa unaamini kuwa kugusa gari kutakuponya ni kweli. Unachoamini kina nguvu”
@bibi_toya “Gari alilonunua kwa mchango wao mdogo..na jasho. Na sasa inabidi wamkimbilie ili wapate baraka waliyochangia. Sawa sawa.”
@ ms_leemart “Tatizo baadhi ya watu sasa wanamwabudu mtu wa Mungu kuliko Mungu mwenyewe.”