logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Huddah: Katika maisha hata baada ya kupata kila kitu unachofukuzia, ukifa unaacha vyote!

"Viongozi wetu wana nafasi nzuri sana kwa ajili yao kule jehanamu," Huddah alisema.

image
na Davis Ojiambo

Burudani24 July 2024 - 12:35

Muhtasari


    Mwanamitindo Huddah Monroe amefunguka kwamba hakuna jambo humshangaza katika maisha kuhusu mwisho wa maisha yenyewe.

    Kupitia ukurasa wake wa Instagram, mwanasosholaiti huyo amedai kwamba Kenya inafaa kuwa moja ya nchi ambazo wananchi wake hawafai kuishi maisha yenye changamoto kutokana na utajiri ambao taifa hli linalo.

    Huddah alisema kwamba Kenya ina utajiri mkubwa ambao umekaliwa na watu wachache ambao hawakumbuki dhana kwamba maisha huisha.

    Huddah anadai kwamba ni wakati viongozi wajue kwamba hata ukikalia mali kiasi kipi, maisha yanapofikia mwisho wake unayaaga na kwenda akhera bila kitu.

    “Jambo la kushangaza zaidi kuhusu maisha ni kwamba baada ya kupata kila kitu kwenye utajiri, bado utakufa siku moja na hutaenda na kitu. Ambacho ningependa kuomba serikali ni kujenga hospitali zene haiba ya kisasa. Ili wakati watakapozeeka na kuwa wayonge, badala ya kuabiri ndege kwenda kutafuta matibabu katika mataifa ya wakoloni wao kama marafiki zao waliokufa, watapata huduma za matibabu nyumbani,” Huddah alishauri.

    Huddah bila kubeta alimtaka rais wa sasa kutumia nguvu zake kabla hajazeeka kubadilisha dhana na kuleta mabadiliko ambayo viongozi wakongwe wengine waliotangulia mbele za haki hawakuweza kufanya kwa taifa hili.

    “Ruto na wenzake wako na nguvu sasa lakini hawawezi kuzuia kuzeeka wala magonjwa ya uzeeni. Fanyeni kitu ambacho kina Moi na wenzake walishindwa kufanya. Hatuhitaji mahoteli mengi na majumba,” Huddah alifoka.

    Mrembo huyo mjasiriamali wa bidhaa za urembo alitema nyongo yake zaidi akisema kwamba imekuwa kawaida kwa viongozi kuiba mali ya umma akisema kwamba viongozi wengi wana nafasi nzuri tu imehifadhiwa kwa ajili yao jehanamu.


    RADIO JAMBO FREQUENCIES

    Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


    logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved