MALKIA wa muziki wa Reggae kutoka taifa la Jamaika,
Etana ameonyesha kutofuraiswa kwake baada ya shoo yake kugongana na shoo ya
Diamond Platnumz kupelekea kusitishwa.
Etana kupitia ukurasa wake wa X, alisema kwamba kuna
baadhi ya watu wenye nguvu ambao walihakikisha shoo yake haifanyiki licha ya
kuanza kupigiwa debe miezi kadhaa iliyopita.
Mrembo huyo ambaye aliona shoo yake Jumamosi usiku
ikipigwa breki, alisema kwamba kuna watu walihakikisha wanamkatisha tamaa kwa
kuandaa shoo nyingine sambamba na yake.
Itakumbukwa shoo ya Etana ilijipata imeratibiwa
wakati mmoja na shoo ya Furaha Fest ambayo mfalme wa Bongo Fleva, Diamond
Platnumz alikuwa miongoni mwa wasanii wakuu kutumbuiza.
“Kuna
mtu amelipa pesa nyingi kuhakikisha shoo yangu usiku wa leo inahujumiwa! Sifurahishwi
na hujuma na niseme wazi sijitokezi kwenye show ya Diamond Platinumz!!!!! Yote
ni poa,” Etana alisema kwa sehemu.
“Onyesho
langu la Desemba. 7 lilikuwa likipigiwa debe muda mrefu kabla ya mtu kuibuka na
onyesho la Diamond Platnum siku moja na katika eneo moja,”
aliongeza.
Etana alisema kwamba alipokea kwa maskitiko makubwa
kuwa shoo yake imetolewa kafara kwa ile nyingine kwani hakuna vile shoo zote
mbili zingefanyika katika eneo vmoja.
“Kisha
ghafla nasikia maonyesho mawili hayawezi kufanyika katika ENEO MOJA kutoka kwa
mamlaka na show yangu usiku wa leo haiwezi kutokea.”
Mrembo huyo alihoji ni kwa nini yeyote anayejaribu
kufanya hivyo anaogopa tu yeye mwanamke mmoja tu kwa kupanga ratiba ya wasanii
wengine kutumbuiza.
“Siasa na maigizo haya yote kwa msichana
mmoja. Nashangaa ni nani yuko nyuma ya yote. Kwa nini unaogopa show moja na
mwanamke mmoja?” Alihoji.
Hata hivyo, baada ya shoo ya Etana kupigwa breki
ghafla, taarifa zinadai kwamba Diamond pia hakuweza kutumbuizia mashabiki
katika Furaa Fest na aliondoka jukwaani ghafla.
Msanii huyo anaarifiwa kuondoka Jukwaani baada ya
kugongana na msanii wa humu nchini Willy Paul ambaye pia aliratibiwa kutumbuiza
kabla yake.