MBUNGE wa Kapseret,
Oscar Kipchumba Sudi ameonyesha furaha yake baada ya chuo kimoja cha kibinafsi
kutambua mchango wake katika uongozi na kumtunuku shahada ya uzamivu katika
uongozi na usimamizi.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook,
Oscar Sudi alirundika picha akiwa amevalia joho la mahafali katika chuo hicho
na kufichua kwamba alitunukiwa shahada ya kiheshima katika uongozi.
Alishukuru chuo hicho
kwa kutambua mchango wake katika uongozi na usimamizi na pia kuchukua nafasi
hiyo kuwahongera mahafali wenzake kwa juhudi zao kulipa siku ya kufuzu kwao
katika chuo anuwai cha Eldoret.
“Nina heshima kubwa
kupokea Shahada ya Heshima ya Uzamivu katika Uongozi, Utawala, na Usimamizi
kutoka Chuo Kikuu cha Kikristo cha Northwestern katika The Eldoret National
Polytechnic. Utambuzi huu unasisitiza asili isiyo na kikomo ya elimu-kweli
haina mipaka. Kwa wahitimu wa mwaka huu, pongezi kwa hatua hii ya ajabu. Safari
zako za mbele ziwe na athari na za kutia moyo,”
Sudi alichapisha.
Mashabiki wa mbunge huyo
mtetezi mkali wa sera za serikali ya siku walifurika kwenye maoni na kumpa
hongera za dhati kwa juhudi zake zilizotambulika na kutuzwa.
Haya hapa baadhi ya
maoni;
Sialo Kimiring: “Hongera
kwa utambulisho huu unaostahili! Mafanikio yako yanaangazia uongozi wako na
kujitolea kwako. Nakutakia athari na msukumo unaoendelea katika juhudi zako
zote!”
Alvin Njoroge: “Hongera.
Unanitia moyo sana na hadithi yako ya maisha, Mungu akubariki, Siku moja
tutakutana.”