MSANII NA MJASIRIAMALI Esther Akoth Kokeyo maarufu kama Akotee ameahidi kutoa msaada wa kimasomo kwa watoto 4 mayatima ambao picha yao ya kutia huruma wakiwa kwenye jeneza la marehemu mzazi wao ilevutia hisia nyingi na nzito mitandaoni.
Watoto hao wadogo 4 walisimamishwa mbele ya jeneza la
mzazi wao kwa picha ya mwisho ya kumbukumbu, na picha hiyo imevutia hisia
nyingi na nzito miongoni mwa watumizi wa mitandao.
Hata hivyo, haijulikani hafla hiyo ya mazishi hayo ya
kutia huruma ilifanyika wapi, lakini watu wengi wameomba msaada wa jinsi
wanaweza fikia familia hiyo changa iliyoachwa.
Mmoja wa watu ambao wameomba kusaidiwa kufikia watoto
hao ni Akothee ambaye ameahidi kuwapa msaada wa kimasomo watoto hao katika
shule yake ya Akothee Foundation.
Msanii huyo aliomba mtu yeyote anayeweza kumpa msaada
wa kuwafikia kujitokeza, akisema kuwa japo shule yake si ya bweni, lakini
angeomba kuwasaidia mradi tu wawe na mtu angalau mmoja kutoka kwa uko atakayewatunza
ili kufikia masomo kwa kutwa.
“Moyo
wangu umeumizwa na kuona watoto hawa. Je, kuna yeyote aliye na habari kamili au
maelezo kuhusu jinsi tunavyoweza kusaidia? Ingawa shule yangu bado si taasisi
ya bweni, ikiwa wana mlezi au mwanafamilia aliyesalia, niko tayari kuwahifadhi
chini ya uangalizi na mwongozo wa ndugu zao wa damu.”
“Nitatoa
chakula, elimu, malazi, matibabu, na usaidizi mwingine wowote wa kimama
wanaohitaji,” Akothee aliahidi.
“Walakini,
ni muhimu kwamba waambatane na mtu wa familia. Ulimwengu unaweza kuwa wa
kikatili sana, lakini kwa pamoja, tunaweza kuleta mabadiliko. Mungu akubariki
mwaka huu kwa kugusa mioyo,” aliongeza mama huyo wa
watoto 5.