
MSANII Mbosso Khan yuko mbioni kuondoka katika lebo ambayo imemkuza ya WCB Wasafi muda wowote kutoka leo hii.
Haya ni kwa mujibu wa rafiki na chawa wa karibu wa bosi wa
lebo hiyo, Baba Levo ambaye amefichua kwamba Diamond Platnumz tayari
ameshalipitisha suala la msanii huyo kuondoka.
Baba Levo alifichua kwamba Diamond amemruhusu Mbosso kuondoka
bila kulipia gharama ndefu kama watangulizi wake – Rayvanny, Harmonize na Rich
Mavoko.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo kutoka kwa Baba Levo, Diamond
amemsamehe Mbosso gharama hizo zote na kumruhusu kuondoka bila kulipia hata
senti kutokana na nidhamu kubwa ambayo ameionyesha tangu ajiunge na WCB.
Levo alisema kwamba Mbosso ametamkiwa Baraka zote na bosi
wake kuondoka ili kuendelea kuipambania nyota yake kimuziki nje ya WCB Wasafi.
“Kutokana na heshima
kubwa ya Mbosso kwa Diamond na viongozi wa WCB, Lukuga [Diamond] amemfungulia
milango Mbosso akajitafutie mwenyewe bila kulipa chochote WCB.”
“Nidhamu Kubwa Ya MBOSSO
Imemfanya @diamondplatnumz Amsemehe MAMILIONI YA PESA Na Kumpa UHURU WA KWENDA
KUPAMBANA NNJE YA WCB,” Baba Levo aliakisi.
Aidha, chawa huyo wa Diamond alizidi kutoa taarifa zaidi
akifichua kwamba Diamond na uongozi wake baada ya kuondoka kwa Mbosso watasaini
wasanii wapya 9.
“Hii Inawapa NAFASI WCB KUSAINI WASANII WENGINE WAPYA MWAKA
HUU 2025,” Baba Levo alifichua.
https://www.instagram.com/p/DFat_yiNP4L/
Mbosso, ambaye jina lake halisi ni Mbwana Yusuph Kilungi alianza
kazi yake ya muziki mnamo 2013 kama mwanachama wa Yamoto Band, ambapo alienda
kwa jina la kisanii "Maromboso".
Mnamo 2018, alisaini na WCB Wasafi, lebo ya rekodi
iliyoanzishwa na Diamond Platnumz.
Mbosso ametoa vibao vingi vilivyoongoza chati, vikiwemo
"Maajabu", "Picha Yake", "Tamu",
"Tamba" miongoni mwa mashairi mengine mengi na kumfanya kujinafasi
miongoni mwa mastaa tajika wa muziki Afrika Mashariki.
Ikiwa ni kweli ataondoka, basi atakuwa msanii wan ne kugura
lebo hiyo inayoaminika kuwa bora zaidi Afrika Mashariki.
Watangulizi wake katika kuondoka WCB ni pamoja na Harmonize,
Queen Darleen, Rayvanny na Rich Mavoko.
Kuondoka kwake kutamaanisha kwamba Diamond atasalia na
wasanii watatu tu – Zuchu, Lavalava na D Voice ambaye alisajiliwa na WCB
Novemba 2023.