
MSANII wa EMB Records, Bahati Kioko ametoa tamko la kejeli kwa wasanii wengine akisema kwamba kama walishindwa kutengeneza pesa wakati yeye na Willy Paul walikuwa hawapatani basi asahau kuwa Tajiri.
Bahati alikuwa anazungumza katika
video moja akiwa na Willy Paul katika maandalizi ya mwisho kuelekea kuachiliwa
kwa kolabo yao.
Bahati alidai kwamba kama kuna msanii
yeyote aliyeshindwa kuchukua fursa ya bifu lake na Willy Paul kutengeneza pes
abasi atakufa maskini kwani wawili hao tayari wamerekeisha urafiki wao.
Alijipiga kifua akisema kwamba yeye
na Willy Paul ndio wasanii pekee wamekuwa wakishikilia tasnia ya burudani
nchini kwa miaka 10, na kama hiyo haitoshi, ndio tena wameanza upya wakiwa
marafiki.
“Unajua sasa hivi ndio
tumeanza, ni enzi mpya na ujue bado sisi ndio tumekuwa tukishikilia kwa miaka
10 na ndio tunaanza tena. Hivyo kama kuna msanii hakutengeneza pesa huo wakati
ajue sasa atakufa maskini maana sisi tumerudi,” Bahati
alisema huku Willy Paul akimuunga mkono kwamba hii ni enzi ya kuwafuuza wasanii
wa kigeni kutoka kilele cha chati za muziki humu nchini.
Alhamisi, wawili hao ambao wamekuwa
wakihasimiana kwa miaka kadhaa walitangaza kuja Pamoja na kuachia kolabo mbili
kwa mpigo.
Walitangaza kolabo hizo zingeshuka
mapema Ijumaa asubuhi na upekuzi wa haraka, tayari kufikia muda wa kuchapishwa
kwa ripoti hii walikuwa wameachia ngoma ya kwanza kwa jina ‘Paah’.
Ngoma nyingine ambayo wamefanya Pamoja
na ambayo ingeshuka muda sawia inaitwa ‘Keki’.