logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Milka Moraa Amshukuru Pasta Ng’ang’a Kwa Kumwelekeza Kwa ‘Affordable Housing’

“Nashukuru Mungu kwa kuniwezesha nimefika mahali hapa na pili ninashukuru pasta Ng’ang’a kwa kunielekeza huku,"

image
na MOSES SAGWEjournalist

Burudani06 February 2025 - 13:02

Muhtasari


  • Milka Moraa Tegisi alizungumza katika video fupi ambayo ilionwa na meza yetu ya habari akimshukuru pasta Ng’ang’a kwa kitendo hicho kilichojiri kanisani.
  • Tukio hilo lilinaswa pale Moraa alipojongea kwenye mimbari kujieleza masaibu yake kwa mchungaji.

Milka Moraa Tegisi amshukuru Pasta Ng'ang'a kwa kumtaka kuenda kwa affordable housing kupata nyumba

MWANAMKE aliyefukuzwa na mchungaji wa kanisa la Neno Evangelism, James Maina Ng’ang’a hatimaye amevunja kimya kuhusu tukio hilo lililofanyika takribani wiki mbili zilizopita.

Milka Moraa Tegisi alizungumza katika video fupi ambayo ilionwa na meza yetu ya habari akimshukuru pasta Ng’ang’a kwa kitendo hicho kilichojiri kanisani.

Tukio hilo lilinaswa pale Moraa alipojongea kwenye mimbari kujieleza masaibu yake kwa mchungaji.

Alifunguka baina ya machozi akimuelezea Ng’ang’a jinsi nyumba yake ilikuwa imefungwa kwa kudaiwa kodi ya shilingi elfu nane.

Ng’ang’a alimlipua akimwambia kwamba yeye hatoi msaada wa kodi ya nyumba kanisani humo huku akimuelekeza kuenda kwa serikali kupewa nyumba chini ya mpango wa Boma Yangu.

“Si kuna nyumba zimejengwa zinaitwa affordable? Si uende ukae hizo za affordable? Ndio nasema shida ya nyumba usiniletee. Shida ya nyumba enda kwa serikali. Mimi ninashughulika na mambo ya kiroho. Mambo kuhusu pesa, usije hapa ukitarajia pesa,” Ng’ang’a alimlipua

Moraa alizungumzia suala hilo na kumshukuru Ng’ang’a kwa kumuelekeza vizuri kwani hatimaye alikutana na waziri wa ardhi Alice Wahome ambaye alimuandikisha na kumuahidi kupata nyumba chini ya miezi miwili ijayo.

“Nashukuru Mungu kwa kuniwezesha nimefika mahali hapa na pili ninashukuru pasta Ng’ang’a kwa kunielekeza huku, nimechukua mwelekeo sawa, nimefaidika na kusaidika. Nimepata nyumba na ikiwa tayari nitaingia,” alisema.

Awali, waziri Alice Wahome pia alitoa shukrani zake kwa Ng’ang’a akisema kwamba yeye ndiye aliyemuelekeza Moraa kwa mpango wa Boma Yangu japo kwa hasira.

“Lazima pia nimtambue Mchungaji Ng’ang’a kwa kumwelekeza Milka kwenye Nyumba ya bei nafuu, asante sana,” waziri wahome alisema.

Wahome alifichua kwamba nyumba ya Moraa itakuwa tayari ndani ya kipindi cha miezi 2 na akafichua kwamba itakuwa na huduma muhimu kama jikoni, choo na hata bafu.

“Katika muda wa miezi miwili, Milka sasa anatazamiwa kumiliki nyumba ya kujitegemea katika Mukuru Site, ambayo imekamilika na huduma muhimu, ikiwa ni pamoja na jiko, bafu na choo,” waziri Wahome alisema.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved