
MWANASOSHOLAITI Vera Sidika ameonyesha kutoridhishwa kwake na huduma ya ukandaji ambayo alifanyiwa akwa nchini Marekani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Ijumaa, Sidika
alilalamika akisema kwamba alifanyiwa masaji katika eneo moja nchini Marekani
na licha ya kulipishwa kiasi kikubwa cha fedha, hakuridhia na huduma hiyo.
Sidika alionesha risiti ya malipo kwa huduma ya kukandwa –
shilingi 42,000 pesa za Kenya ambapo baadae aligundua kuwa huduma ya kukandwa
haikumridhisha.
“Masaji hii ilinigharimu shilingi 42,000 pekee lakini kusema kweli ilikuwa duni zaidi. Sasa nahitaji masaji nyingine ili kupona kutonana na hii,” Vera Sidika alichapisha.
Sidika ambaye amekuwa akichapisha picha akizuru Maeneo mbalimbali
ya haiba ya kipekee nchini Marekani alionekana kupendelea huduma za kukandwa
ambazo anapata humu nchini.
Wiki chache zilizopita, sosholaiti Vera Sidika alichapisha
picha zake akila kwenye mkahawa mmoja na kuonesha pesa taslimu na risiti ya
pesa nyingi.
Sidika anajulikana kwa maisha yake ya kifahari na ameonekana
akionyesha mavazi ya wabunifu, likizo za kifahari, na mali za kifahari.
Katika chapisho moja, alishiriki kwamba alikuwa ametoka kwa
chakula cha mchana na akaeleza kwa utani chakula hicho kama "chakula cha
Kenya" anachokipenda zaidi.
Katika chapisho jingine, alionyesha risiti ya mlo wa jioni
uliogharimu KSh 198,000.
Onyesho la Sidika lilivuta hisia na mashabiki walimiminika
mitandao ya kijamii kwa hisia. Wengine walihoji ikiwa onyesho lake lilikuwa la
kufurahisha au kujionyesha bila madhara.
Sidika alipata umaarufu mwaka wa 2012 aliposhirikishwa katika
wimbo wa P-Unit "You Guy". Mnamo 2014, alionekana katika single ya
Prezzo, "My Gal".