
NDEGE ya shirika la ndege la United Airlines iliyoondoka Marekani kuelekea Uchina mwishoni mwa juma lililopitya ilibidi ibadilishe njia na kurudi ilikotoka kwa sababu rubani alisahau kubeba pasipoti yake, CNN wameripoti.
Ndege hiyo, ikiwa na abiria 257 na wafanyakazi 13, iliondoka
Los Angeles mnamo Machi 22 saa nane mchana na kuanza safari ya saa 13½ hadi
Shanghai, Uchina.
Takriban saa mbili baada ya safari ya ndege, hata hivyo,
Boeing 787-9 ilibidi kugeuka na kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
San Francisco (SFO) kwa sababu rubani "hakuwa na pasipoti yake",
alisema msemaji wa United katika taarifa.
Data kutoka kwa tovuti ya kufuatilia safari za ndege ya
Flightradar24 ilionyesha ndege hiyo ikiruka kutoka Los Angeles juu ya Bahari ya
Pasifiki kabla ya kugeuka na kurudi California.
Kufuatia tukio hilo, abiria Paramjot Singh Kalra alichapisha
kwenye X: "UA198 iligeukia SFO kwa sababu rubani alisahau pasi yake ya
kusafiria? Sasa ilikwama kwa saa 6+. Haikubaliki kabisa, ni fidia gani mnayotoa
kwa uzembe huu wote?"
Shirika la ndege lilijibu kwa kuomba radhi kwa
"usumbufu wa usafiri usiotarajiwa" na likatoa usaidizi kwa abiria kwa
wakala.
Msemaji wa shirika hilo la ndege alisema shirika la ndege
lilikuwa limepanga wafanyakazi wapya kuwasafirisha abiria walioathirika hadi
wanakoenda jioni ya Machi 22.
Abiria pia walipewa vocha za chakula na fidia. Wafanyakazi
wapya waliondoka saa tatu usiku na kutua Shanghai karibu saa sita nyuma ya
ratiba, kulingana na CNN.