logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Babaiko Wanandoa Wakilazimishwa Kukaa Karibu Na Abiria Aliyekufa Kwenye Ndege

Wafanyakazi hao walianza kuchukua blanketi kutoka kwa mwili na kuikagua wakati jamaa na mkewe walikuwa wameketi hapo, kumaanisha aliona uso wa mwanamke huyo maiti.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Habari25 February 2025 - 16:50

Muhtasari


  • Wafanyakazi waliona kulikuwa na viti wazi pande zote mbili za wanandoa na wakawaomba wasogee ili kutoa nafasi kwa mwili.
  • Mwanamke aliyekufa aliwekwa kando ya Bw Ring, na kufunikwa kwa blanketi kwa saa nne zilizosalia za safari ya kuelekea Doha.

Abiria wakiingia kwenye ndege

WANANDOA walionekana kuchanganyikiwa kisaikolojia baada ya kulazimishwa kuketi karibu na abiria aliyekufa katika safari ya saa kadhaa kutoka Melbourne, Australia kuelekea Venice, Italia wamesimulia tukio hilo.


Wanandoa hao waliokuwa na kiwewe walieleza kwamba abiria huyo mwanamke alikufia ndani ya ndege hiyo na kuletwa karibu na nafasi walikokuwa wameketi.


'Kwa bahati mbaya, mwanamke huyo hakuweza kuokolewa, jambo ambalo lilihuzunisha sana kutazama,' mwanamume aliiambia kipindi cha A Current Affair.


'Walikwenda kujaribu kumsogeza, wakateremsha kiti hiki ... na wakamweka kwenye kiti na kujaribu kumsukuma kuelekea business class. Lakini alikuwa mwanamke mkubwa kabisa, na hawakuweza kumpitisha kwenye njia hiyo.'


Wafanyakazi waliona kulikuwa na viti wazi pande zote mbili za wanandoa na wakawaomba wasogee ili kutoa nafasi kwa mwili.


Mwanamke aliyekufa aliwekwa kando ya Bw Ring, na kufunikwa kwa blanketi kwa saa nne zilizosalia za safari ya kuelekea Doha.


Kwa Bi Colin, ambaye ni msafiri mwenye wasiwasi, mkasa huo ulikuwa wa kuhuzunisha.


'Mume wangu alipogeuka na kusema, "sogea, sogea", nilishtuka sana na nikasema, "watamweka huko?",' alisema.


Kwa bahati nzuri, mwanamke aliye na kiti cha ziada katika safu nyingine alimwalika Bi Colin kuketi naye baada ya kudai wafanyakazi wa cabin walishindwa kutoa kuwahamisha mbali zaidi na mwili.


Ili kufanya mambo kuwa mabaya zaidi, wanandoa hao walilazimika kusubiri hata baada ya ndege kuruka Doha wakati polisi na maafisa wa matibabu wakipanda.


Bw Ring alisema wafanyakazi hao walianza kuchukua blanketi kutoka kwa mwili na kuikagua wakati yeye na mkewe walikuwa wameketi hapo, kumaanisha aliona uso wa mwanamke huyo maiti.


"Siamini walituambia tubaki... haikuwa nzuri," alisema.


'Wana wajibu wa kuwajali wateja wao na wafanyakazi wao, tunapaswa kuwasiliana ili kuhakikisha, unahitaji msaada, unahitaji ushauri nasaha?’


Wenzi hao walieleza kwamba tukio hilo liliwaathiri pakubwa na likizo yao huko Venice ambayo walitarajia kuifanya ya kukumbukwa.


 


'Sijui kwa hakika jinsi ninavyohisi na ningependa kuzungumza na mtu ili kuhakikisha kuwa niko sawa.'


Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved