
Mwezi huu wa Januari,2025 umedhihirisha kuwa mwezi wa maafa na mikasa ya ajali za ndege chini ya mwezi mmoja ajali sita za ndege zimeshuhudiwa kote duniani na kuua zaidi ya watu mia moja.
Kati ya hizi ajali, mbili zilishuhudiwa nchini Kenya ikiashiria tu hali ngumu ambayo wafanyakazi wa ndege na Marubani wanakabiliana nazo.
Ajali ya hivi punde ilitokea eneo la Naivasha ambapo watu wawili mwanamume na mkewe walifariki baada ya ndege yao kuanguka. Polisi walisema huenda ajali hiyo ilisababishwa na hali mbaya ya anga. Ajali nyingine ilitokea nchini Marekani Januari tarehe 30,2025 ambapo helikopta ya jeshi na ndege ya abiria ziligongana mjini Washington D.C na kuisababisha vifo vya watu 67.
Ndege ya shirika la merica Airline ambayo ilikuwa inajaribu kutua katika uwanja wa kitaifa wa Ronald Reagan iligongana na ile kijeshi ambapo ndege zote zilianguka Mto Potomaki.
Siku hiyo hiyo nchini Kenya aina ya ndege nambari ya usajili Cessna 185 5Y -BVL ilianguka katika Kedong karibu na Naivasha siku ya alhamisi jioni Januari 30,2025 saa 5:14pm ndege iliyokuwa imetoka katika anga tua ya Willson Airport Nairobi ambapo Rubani Mbaruku alikuwa amebeba watu wawili ambao walipoteza maisha yao papo hapo ajali ambayo iliripotiwa, asasi husika za usalama ziliarifiwa ambapo uchunguzi unaendelea kubaini chanzo cha ajali hiyo.
Mamlaka ya ndege nchini Kenya (KCAA) imedhibitisha kupokea habari hiyo ikishirikiana na timu ya kushughulikia majanga nchini pamoja na ushirikiano wa taasisi za ajali angani ili kutegua kitendawili hicho.Kwingineko kule Venezuela Januari 29,2025 aina nyingine ya ndege nambai ya usajili S550 ndege ya biashara ilihusika katika ajali muda mfupi tu baada ya kupaa kutoka kwa uwanja wa Generalissimo Francisco Miranda Caracas Venezuela ambapo wafanyakazi wa ndege waliaga dunia.
Kule Sudani Kusini ajali nyingine ya ndege ilifanyika tarehe 29 Januari,2025 ambapo ndege kwa jina Beechcraft 1900D iliyokuwa imebeba mafuta kutoka Rabkona Kaunti ilianguka muda mchache tu baada ya kupaa,ndege hiyo ilikuwa na watu 21 waliokuwa wameabiri ndege hiyo ambapo manusura wawilli walipatikana na ambapo wako katika hali mbaya wanaopoendelea kupokea matibabu.
Korea kusini mnamo januari 28, 2025 moto ulizuka katika ndede ya Busan A321 katika uwanja mkuu wa Busan Gimhae moto ukioanzia nyuma ya ndege ambapo ilisababisha kuondolewa kwa abiria 170 na wafanyakazi 6 ambapo iliripotiwa kuwa watu wawili walipata majeraha hii ajali inatokea tu baada ya ajali nyingine kutokea mnamo Desemba 2024 ambapo iliua watu 179.
Kule Brazili ajali ya ndege ilishuhudiwa Januari 9 ,2025 ambapo ndege nambari ya usajili Cessna 525 iliyokuwa inajaribu kutua katika uwanja wa Gastao Madeira ilipo lipuka baada ya kutua watu wawili walifariki akiwemo Rubani na wengine wanane kujeruhiwa vibaya wakati ambapo dunia inaangazia maafa na ajali hizii za ndege kuna mikakati ambayo inaendelea kuhakikisha kuwa Marubani wanapata mafunzo ya kutosha. mwezi huu wa Januari utakumbukwa kuwa mwezi mbovu katika taasinia ya anga kwa jumla duniani.