
KIJANA mrefu zaidi humu nchini Bradley Marongo maarufu kama Gen Z Goliath ama Bradley Mtall amefunguka kwamba yeye kwa sasa ni Muislamu baada ya kile alichodai kwamba amebadili dini hivi majuzi – hivyo anaweza oa wanawake hadi 4.
Akizungumza moja kwa moja kwenye runinga
ya NTV, Bradley Marongo, alionyesha uhodari wake baada ya kujaribu kurusha
mistari yake kwa mtangazaji wa kipindi Amina Abdi Rabar.
Bradley alifunguka kwa Amina kwamba
amekuwa akimtolea jicho la kumtamani na mara kwa mara hata kabla wakutane
kwenye studio za NTV, alikuwa akimsumbua meneja wake – Director Trevor –
kumtafutia jinsi ya kuwasiliana na Amina.
Bila kupiga kona na kuenda njia ndefu,
Bradley alimkabili Amina moja kwa moja na swali la kutaka kujua kama ana mume
au la, akiwa na lengo la kutaka kujaza hilo pengo kama jibu lake lingekuwa la!
“Unajua huwa nasumbua Trevor kila
siku nikimwambia Trevor nitafutie namba ya Amina. Namwambia Trevor mimi nataka Amina,
nimemcrushia Amina. Trevor aliniambia Hapana Amina ako na bwana, sasa ndio
nataka uniamie leo uko na bwana ama Hapana?”
Bradley Marongo alimuuliza Amina bila kupepesa jicho.
Hata hivyo, Amina alimvunja moyo kwa
kumwambia kwamba yeye ni mke wa mtu lakini Bradley hakukaa kinyonge, alijitetea
kwamba yeye sasa hivi ni muislamu na ana uwezo wa kuishi katika ndoa ya mitala.
“Sasa unajua mimi ni Muislamu na
tunaruhusiwa kuoa bibi watatu hadi wanne. Jina langu la Kiislamu kwa sasa ni
Ishmael. Lakini hata kama Amina uko na mtu, unajua hata kugongewa ni constant,”
Bradley alimshinikiza zaidi Amina kukubali ombi lake.
Kijana huyo anayejidai kuwa na urefu wa
zaidi ya futi 8 alijizolea umaarufu mwaka jana, shukrani kwa harakati za
maandamano ya vijana wa Gen Z ambapo alionekana na kuvutia umakini wa wengi.
Tangu wakati huo, Bradley amekuwa kipenzi
cha wengi kiasi kwamba kila anayekutana naye anaingiwa na uchu wa kutaka kupiga
picha naye.
Amekuwa akisimamiwa na Director Trevor
ambaye kupitia kwake Bradley amepata dili kibao za kuwa balozi wa mauzo ya
kampuni za bidhaa mbalimbali ndani na nje ya Kenya.