logo

NOW ON AIR

Listen in Live

2 wakamatwa makaburini wakiiba vibao, misalaba ya chuma kuuza kama vyuma chakavu

Makumi ya bidhaa za makaburi zinazodaiwa kuharibiwa na vijana hao zilisombwa mbele yao na kupigwa picha nao kama ushahidi.

image
na MOSES SAGWEjournalist

Burudani23 April 2025 - 12:45

Muhtasari


  • Makumi ya bidhaa za makaburi zinazodaiwa kuharibiwa na vijana hao zilisombwa mbele yao na kupigwa picha nao kama ushahidi.
  • Chapisho hilo lilizua wasiwasi na mjadala mkubwa mtandaoni, huku watu wengi wakienda kwenye sehemu ya maoni ili kushiriki mawazo na maoni yao.

Vijana waliokamatwa wakiiba makaburini//Screegrab-X

VIJANA wawili wenye umri wa makamo wametiwa mbaroni wakitekeleza shughuli za kuharibu vifaa vya marehemu makaburini kwa ajili ya kwenda kuuza kama vyuma chakavu.

Video ya tukio hilo ilisambazwa kwenye mtandao maarufu wa kijamii, zamani Twitter.

Katika video hiyo, vijana hao waliofumaniwa na wananchi ambao walikuwa wamechoshwa na visa vya kuharibiwa kwa makaburi ya wapendwa wao waliwashurutisha vijana hao kushikilia mabango hayo ya chuma kwa ajili ya kupigwa pcha.

Makumi ya bidhaa za makaburi zinazodaiwa kuharibiwa na vijana hao zilisombwa mbele yao na kupigwa picha nao kama ushahidi.

“Vijana wawili walinaswa na wenyeji kwenye makaburi kwa madai ya kuiba mbao za makaburi ili kuziuza kama chakavu. Wawili hao, wanaoshukiwa kuwa wafanyabiashara wa vyuma chakavu wa eneo hilo walipigwa viboko vikali kabla ya kuandamana na nyara zao,” Maelezo ya chapisho hilo yalisema.

Chapisho hilo lilizua wasiwasi na mjadala mkubwa mtandaoni, huku watu wengi wakienda kwenye sehemu ya maoni ili kushiriki mawazo na maoni yao.

Tazama baadhi ya maoni hapa chini:

@ThemGoTalk1: "Fikiria kuiba kutoka kwa wafu na bado huna dhamana ya begi. Hata mababu wanatikisa vichwa vyao."

@KSnetne: "Kuhamia makaburini kumeharibika! Kuiba chuma kutoka makaburini? Hata mizimu isingejisalimisha kwa shamrashamra hizo. Natumai kupigwa kulikuja na somo la bure kuhusu kuheshimu wafu, na chaguo bora zaidi za kazi."

@Emmanue48407309: "HII NI AJABU na CHUKIZO! Wanathubutuje hata kufikiria kuwafanyia wafu hivi? Ni mwiko kuchafua makaburi katika jamii yetu. Hakuna heshima kabisa kwa kumbukumbu ya wafu. Wanapaswa kupewa adhabu kali za jela!"

 

 

 

 

 

 

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved