logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kwaheri Gwiji! Leonard Mambo Mbotela Kuzikwa Leo, Jumamosi Katika Makaburi Ya Lang'ata

Spika Wetang’ula alisema inavunja moyo kwa Mbotela kuzikwa katika makaburi ya Lang’ata.

image
na Samuel Mainajournalist

Yanayojiri15 February 2025 - 08:25

Muhtasari


  •  Hafla ya maziko ya mtangazaji huyo nguli inatarajiwa kufanyika saa nne alfajiri katika makaburi ya Lang'ata. 
  •  Ibada ya ukumbusho ya mtangazaji huyo mashuhuri ilifanyika Ijumaa katika Kanisa Kuu la All Saints Cathedral.

Seneta Edwin Sifuna alihudhuria ibada ya ukumbusho ya Leonard Mambo Mbotela mnamo Februari 14, 225

Marehemu mwanahabari mkongwe Leonard Mambo Mbotela atazikwa leo Jumamosi, Februari 15.

 Hafla ya maziko ya mtangazaji huyo nguli inatarajiwa kufanyika saa nne alfajiri katika makaburi ya Lang'ata. Wanafamilia, marafiki wa karibu, na baadhi ya watu mashuhuri nchini Kenya wanatarajiwa kuhudhuria hafla hiyo.

 Mbotela alifariki mnamo Februari 7, 2025.

 Mwanahabari huyo mkongwe alikuwa hajisikii vizuri kwa muda na alikata roho mwendo wa saa tatu unusu siku ya Ijumaa wiki iliyopita.

 Ibada ya ukumbusho ya mtangazaji huyo mashuhuri ilifanyika Ijumaa katika Kanisa Kuu la All Saints Cathedral kuanzia saa nane mchana.

 Familia, marafiki wa karibu, wafanyakazi wenzake wa zamani, wanasiasa na watu wengine mashuhuri walihudhuria ibada ya kumbukumbu iliyofanyika kumuenzi marehemu.

 Mnamo Alhamisi, spika Moses Wetang’ula alisema inavunja moyo kwa mtangazaji Leonard Mambo Mbotela kuzikwa katika makaburi ya Lang’ata.

 Akizungumza wakati wa kikao cha Bunge, spika alipendekeza haja ya nchi kuwa na makaburi maalumu ya kuzika mashujaa wa kitaifa.

 Weta aliliomba Bunge kusimama na kuzingatia dakika za ukimya katika kumbukumbu ya mtangazaji aliyefariki.

 “Nchi inahitaji sehemu maalum ya shujaa kuzika watu kama mtangazaji Leonard Mambo Mbotela, inakatisha tamaa kusikia kwamba tunaenda kumzika mtangazaji Leonard Mambo Mbotela katika makaburi ya Lang’ata; pengine kaburi lake litakuwa juu ya kaburi likijua jinsi eneo hilo lina watu wengi,” Wetang’ula alisema.

 Mwanahabari huyo nguli alisifika kwa kipindi chake maarufu cha redio na TV Je Huuu ni Ungwana?, kilichopeperushwa kwenye redio na TV za KBC.

 Kipindi hichi kilifurahia kupeperushwa kwa takriban miaka 55.

 Mbotela alifanya kazi kwa muda mfupi na Kenya Weekly News na East African Standard kabla ya kujiunga na KBC.

 Mwanahabari huyo mkongwe alizaliwa Freetown, Mombasa, mwaka wa 1940 na James na Aida Mbotela. Alikuwa mzaliwa wa kwanza katika familia ya watoto wanane.

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved