
Mwimbaji na mjasiriamali maarufu wa Marekani Kanye West amejitolea kumsaidia rapa mwenzake Kodak Black baada ya video yake ya kutia wasiwasi kuonekana mtandaoni.
Katika video iliyosambazwa mitandaoni, Kodak Black alionekana akiwa amekalia katikati ya barabara huku akila kuku kutoka kwenye sahani ya kubebea chakula.
Tukio hili lililizua wasiwasi mkubwa miongoni mwa wafuasi na mashabiki wa muziki duniani.
Video hiyo ilienea kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, na wengi walijiuliza kuhusu hali ya kiakili ya Kodak Black, hasa kwa kuwa rapa huyo alionekana akiwa katika hali ya kushangaza na kutokuwa na uangalizi wa kutosha. Wengi walijali kuhusu usalama wake na kuhoji kama alikuwa anahitaji usaidizi.
Kufuatia tukio hilo, Kanye West alijitokeza na kutoa msaada kwa Kodak Black.
"Najiandaa kuenda Atlanta kumsaidia kaka yangu, tuombee,” Kanye West aliandika kwenye mitandao ya kijamii.
Kanye aliongeza kwamba alikuwa tayari kusaidia kwa njia yoyote ile na kumfungulia milango ya msaada, ikiwa ni pamoja na kumsaidia kiakili na kielimu.
Kodak Black, ambaye amezoea kuwa kwenye vyombo vya habari kwa matukio mbalimbali yenye utata, alithibitisha msaada wa Kanye West na kumshukuru kwa kutaka kumsaidia.
Alisema kuwa Kanye ni mtu wa kweli na alielezea furaha yake kwa hatua aliyochukua Kanye.
“Nashukuru kwa msaada wako Kanye, wewe ni mtu wa kweli,” alisema Kodak Black katika ujumbe wake wa shukrani.
Aidha, Kodak aliongeza kuwa anatarajia kufanya kazi na Kanye West katika miradi ya muziki katika siku zijazo.
Pia alielezea shauku yake ya kushirikiana na rapa huyo maarufu kwa mara nyingine tena.
Huu ni mfano mwingine wa jinsi wasanii wakubwa wanavyoweza kushirikiana na kusaidiana, na pia inaonyesha nguvu ya mitandao ya kijamii katika kuibua hali za wasanii na watu maarufu, ambao mara nyingi wanakutana na changamoto mbalimbali, za kiakili na kisaikolojia.