
MWANAMUME mwenye umri wa miaka 43 amehukumiwa kifungo cha miaka 14 jela baada ya kupatikana na kosa la kuvua mpira wa kinga bila ridhaa ya mrembo wake wakati wa kufanya mapenzi.
Mwanamume huyo aliyetambulishwa kwa jina moja tu la Lawrence katika
mahakama moja jijini London, alikutana na mrembo, 32, katika programu ya
uchumba mitandaoni mnamo Julai 2021 wakati safari yao ya mapenzi ilipoanza.
Baada ya kuchumbiana na kuzoeana kwa muda, wawili hao
walikubaliana kukutana nyumbani kwa mrembo huyo na kukubaliana kufanya mapenzi,
japo mrembo alisisitiza Lawrence kutumia kinga.
Mrembo huyo aliiambia mahakama kwamba aligundua wakati wa
kujamiiana, Lawrence alivua kondomu kisiri na baada ya kumaliza tendo, Lawrence
alimtaarifu kwamba alikuwa mwathirika wa virusi vya UKIMWI.
Dai la kuwa Lawrence alikuwa mwathirika wa virusi baadae
lilipatikana kuwa uongo lakini alikutwa na hatia ya kumpa usumbufu wa kiakili
mrembo kwa kumdanganya.
Pia, Lawrence aligundulika kuwa alitumia anwani ya uongo na
taarifa ya benki, na pia kutumia simu ya kulipia kabla ili kujaribu kuzuia
kugunduliwa na polisi.
Pia alidai kuishi katika nyumba ya mamilioni ya pauni, lakini ukweli alikuwa akiishi katika ghorofa ya kawaida, Maelezo hayo yalisomeka kwa mujibu wa London Evening Standard.
Baraza la mahakama lilimpata na hatia ya kubaka mnamo
Oktoba, na pia alikiri kosa la kumnyanyasa mwathiriwa.
Mnamo Februari 2022 alikiri hatia ya mawasiliano mabaya na
vitisho vya kufichua picha ya kibinafsi kwa waathiriwa wawili tofauti.
Lawrence pia alikuwa ametumia jina la uwongo na alikutana na
mwanamke huyo mtandaoni, na akawatisha baada ya kukutana nao.
Kufuatia hukumu yake, Inspekta Mkuu wa Upelelezi jijini
London alisema: "Ningependa kumpongeza mtu huyu aliyenusurika kwa ushujaa
alioonyesha katika kesi hii na ushahidi aliotoa.”
"Hukumu kali iliyotolewa na hakimu inaonyesha wazi
hatari kubwa ambayo mwanamume huyu analeta kwa wanawake.
"Timu ya uchunguzi ilifanya uchunguzi wa kina, wa bidii
na usio na huruma ili kubaini Lawrence na kupata ushahidi wa kumfikisha
mahakamani kuhakikisha kuwa mwathiriwa aliungwa mkono kote.”