
MWANAMKE wa Kenya anayeitwa amezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii baada ya kumkejeli aliyekuwa mume wake, ambaye alichukua mkopo kufadhili harusi yao ya kitamaduni.
Kulingana na mwanamke huyo aliyetalikiwa, mume wake wa zamani
alitumia mkopo wa benki kulipia kila kitu wakati wa harusi yao ya kitamaduni ya
kupendeza, lakini ndoa yao ilidumu kwa mwaka mmoja tu.
Akionekana kumfuma mkuki mume wake wa zamani kwa kile
kilichoonekana kama uamuzi mbaya wa kifedha, alisema kwamba ndoa hiyo
ilivunjika na mume huyo kubaki akilipia deni la mkopo.
Mke huyo ambaye alisema kwa madaha kwamba tayari ameshasonga
mbele na maisha ya kupata mwenzi mpya, alimkejeli Ex wake kwa kubaki na deni la
benki pamoja na riba lakini pia kuuguza moyo kutokana na ndoa kusambaratika.
“Kiwango [cha harusi]
kilikuwa cha chini lakini mimi sikulipia hata senti kwa ruracio yangu. Yeye alilipia
kila kitu kutoka kwa mavazi yangu, mapambo, mshereheshaji, video, chakula na
hata vipodozi vyotealoigharamika yeye.”
“Ile shughuli ilikuwa ghali sana na sasa amebaki akilipia madeni peke yake wakati mimi niko vizuri katika maisha yangu ya kibiashara na pia nina mchumba mpya,” alisema.
Mwanamke huyo alifuta chapisho lake baada ya kukosolewa
vikali na watumiaji wa mitandao ya kijamii ambao walikutana na dhihaka zake
dhidi ya mumewe wa zamani.
Waliokatishwa tamaa zaidi wamemwita mwanamke asiye na
shukrani. Wamependekeza hata alikuwa akisaliti penzi la mumewe walipokuwa bado
kwenye ndoa.