Msanii Harmonize hatimaye ameweka bayana kwamba hayupo pamoja tena na mpezi wake wa awali, Briana.
Kuligana a ujumbe mrefu aliochapisha katika ukurasa wake wa Istagram, Konde alisema kwamba Briana ni mtu mzuri na hana tatizo naye.
Harmonize alisema kwamba chanzo kikubwa cha ndoa yao kusambaratika ni kutokana na hali kwamba alikuwa bado anampenda Frida Kajala na walikuwa wametengana bila ugomvi wowote.
"..Nilimwambia nimetengana na mtu bila kugombana na nampenda sanaa sasa sina uhakika kama nimemove on, lolote linaweza kutokea," Harmoize aliadika.
Aidha alishikilia kwamba hakuwa na uhakika iwapo alikuwa 'amemove on' na lolote linaweza kutokea.
Sababu nyingine ilikuwa kwamba Briana hakuwa tayari kuishi nchini Tanzania wala Harmonize hakuwa tayari kuishi nchini Australia [nyumbani kwao Briana].
Staa huyo alisema kwamba asingetaka kuwepo maswali mengine kuhusu jambo hilo, huku akisisitiza kwamba kwa sasa anapambana kuhakikisha mke wake [Kajala] anarudi.