logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Kuna muda nilifilisika na kukosa hata tone la tumaini - Tems, staa wa muziki

Tems alisema alikuwa akimtegemea shangazi yake kumpatia chakula ii aweze kujikimu.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri23 September 2022 - 09:48

Muhtasari


• Baada ya masomo yake, Tems alisema alirudi mjini Lagos, Nigeria ambapo alipata kazi ya soko ya kidijitali ila ilimpa huzuni na mahangaiko mengi.

Mwanamuziki wa afrobeat wa Nigeria na mteule wa Grammy Temilade Openinyi alimaarufu Tems alifunguka kuhusu maisha yake kabla ya kupata umaarufu.

Alisema alipitia mahangaiko mengi na mapambano ambayo yalimbidi ajikakamue.

Kwenye mahojiano yake na Jalida la British BQ Tems alifafanua maisha yake alipomaliza masomo yake kwenye chuo kikuu cha Monash.

Baada ya masomo yake, Tems alisema alirudi mjini Lagos, Nigeria ambapo alipata kazi ya soko ya kidijitali ila ilimpa huzuni na mahangaiko mengi.

Tems alisema ilimbidi aiwache kazi hiyo ili aweze kuzingatia alichotaka na kupenda kufanya.

Aliongeza na kusema kuwa muziki ulikuwa ndoto yake na ndicho kilichokuwa chanzo chake cha kuiwacha kazi hiyo aliyokuwa akifanya.

Alisema kuwa alipoiwacha kazi ile ndipo alipocharazwa na ukweli wa maisha na mambo yakaanza kuwa magumu.

Mwanamuziki huyo alifafanua jinsi ilivyokuwa ngumu kuitengeneza jina yake ili aweze kupata sifa kwenye sekta ya burudani ya Nigeria.

“Kulikuwa na wakati ambao sikuwa nimefilisika tu, bali sikuwa na tone la tumaini,”alisema.

Tems alisema alikuwa akimtegemea shangazi yake kumpatia chakula ili aweze kujikimu.

“Nilikua na uzoefu wa kuiba chakula,” aliongeza.

Alisema alijipa moyo na kuchagua njia ya tumaini ili aweze kujiinua kwenye sekta yake ya kimuziki na kuweza kutumia nafasi yoyote angeweza kupata.

Ijapokuwa mwanamuziki huyo amewapa wasanii wanaojenga jina lao na sifa, aliweza kusema pia hakujenga ama kukua na siku moja, ilimchukua muda na subira yake ili awe kufika alipo sasa.

Mteule huyo wa Grammy alisema wimbo wake wa kwanza ulipovuma alikuwa amesumbuka sana kifedha.

Kwa sasa Tems ameweza kuwa mteule wa tuzo za Grammy na pia amekua kwenye sekta ya muziki na kuweza kurekodi wimbo na wasanii wakubwa.

 

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved