Moja ya changamoto inayoikabili tasnia ya muziki nchini Tanzania inatajwa kuwa ni rushwa ya ngono.
Mwanamuziki wa siku nyingi Stara Thomas anathibitisha hilo kwa kusema kuwa wanamuziki wa kike ndiyo waathirika wakubwa zaidi. Akiongea na mwandishi wa BBC mkongwe huyo wa muziki wa zuku nchini anasema kuwa ni muda sasa kwa wasanii wa kike kuwa na taaluma ya muziki ili waweze kujisimamia na kukabiliana na tatizo hilo. Mwandishi wa BBC Veronica Mapunda amezungumza naye.