Siku chache zilizopita bendi ya muda mrefu na yenye mafanikio makubwa kimuziki kutoka humu nchini Sauti Sol walitangaza kuwa watafanya shoo yao ya mwisho kabisa kabla ya kila mmoja kujishughulisha na hamsini za kwake.
Sauti Sol walitangaza kwamba kiingili katika shoo hiyo kitakuwa shilingi elfu 20 za Kenya.
Watu mbali mbali walifurika mitandaoni wakitoa maoni yao haswa kuhusu kiwango hicho cha kiingilio ambacho baadhi walikitaja kuwa cha juu sana kwa shoo ya usiku mmoja lakini pia wengine waliwapongeza kwa kiingilio hicho.
Msanii Khaligraph Jones ni mmoja wa wale ambao wanahisi Sauti Sol waliweka bei nzuri ya kiingili akisema kwamba hata alipoona hivyo alihisi kuangushwa nao kwani angetarajia wangeweka kiwango cha juu hadi laki moja.
“Kusema ukweli Sauti Sol waliniudhi sana, Sauti Sol mnaniangusha sana kuweka hiyo bei. Yaani mnaweka aje 20k, si mngeweka hata 100k. Sauti Sol ni wasanii ambao wamefanya kila kitu katika tasnia ya muziki, hawa jamaa ni viongozi wa mfano na wao ndio wasanii wakubwa Zaidi ambao wamewahi kuzalishwa na hii nchi,” Khaligraph alisema.
Khaligraph alisema kwamba yeye shoo yake siku ataiweka kiingilio kitakuwa shilingi 50k bila kujali ni watu wangapi watahudhuria.
“Hata mimi siwezi nikasimama nikasema nimeshinda Sauti Sol, uongo mimi sijawashinda. Mimi siku nitaweka shoo yangu kiingilio ni 50k na itabidi imekuwa hivyo wale watakuja sawa wale hawataki wakae kwa nyumba. Na mimi najua wale watakuja,” alisema.
Khaligraph pia alikuwa na ushauri kwa Sauti Sol;
“Sauti Sol waweke kiingilio cha 100k na tutakuja kuwaona. Mimi nitakuwa tayari kulipa. Mimi wakati wowote wanaweka shoo yao mimi huwa siwaitishi tikiti nakwenda naingia kwa lango na kununua tikiti. Kama hiyo shoo yao nitalipa hiyo 20k na nioneshe watu kwamba hawa jamaa wanastahili kuitisha kiasi hiki cha kiingilio na hata Zaidi kwa sababu Sauti Sol wametuwakilisha pakubwa, tuwape heshima,” alisema.