Mwanasosholaiti Vera Sidika anatarajiwa kukutana kwenye hafla moja na aliyekuwa mume wake Brown Mauzo wikendi hii.
Wawili hao wameratibiwa kuwa wageni maalum katika tamasha moja litakalofanyika Executive Gardens, mjini Mwea. Tangu kutengana kwao, hii itakuwa ni hafla ya kwanza kwa wawili hao kukutana.
Wawili hao, ambao walitangaza kutengana mwishoni mwa Agosti, walionekana kwenye bango moja ambalo pia inashirikisha rapper Khaligraph Jones, mburudishaji wa klabu ya MC Gogo na kikundi cha muziki wa kufoka, Wakadinali.
Haya yanajiri siku chache tu baada ya Vera kuandaa karamu ya kifahari ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwa binti yake wa miaka miwili, Asia Brown, karamu ambayo Vera alisema licha ya kumwalika Brown akikosa kufika.
Kukutana bila kutarajiwa kwa Vera na Brown mjini Mwea kumewafanya mashabiki wa pande zote mbili kutaka kujua jinsi itakavyokuwa jukwaani na pia kutathmini kiwango cha burudani zao hata baada ya kuachana kwa ukali.
Wiki iliyopita uvumi ulienea baada ya Vera Sidika kuonekana akizunguka katika mitaa ya Lagos na baadaye kusherehekea katika jumba la kifahari la Burna Boy, Lagos.
Kulingana na shirika la uvumi la Nigeria, Lamborghini ambayo Vera alionekana akizunguka nayo ni moja kati ya mali ya mwimbaji Burna Boy.
Wiki hii Mauzo alichapisha haya katika kurasa zake za mitandao ya kijamii, kuashiria kuwa huenda amepata mpenzi mwingine.
“Lengo langu ni kujenga na wewe, kukua na wewe na kukuoa. Mimi sikuchumbii kupoteza muda. Ninaona kila ninachotaka kwako mpenzi wangu,” alisema haya hio.