Ndoa nyingi zinavunjika wakati wanawake wanapata ajira -Baba levo

Ndoa za kitambo zilidumu kwa kuwa mila zingefuatwa Baba levo asema

Muhtasari

•Msanii huyu alidokeza kwamba kulingana na tamaduni zilizotumika miaka ya nyuma wanawake hawangeruhusiwa kuajiriwa.

• Jukumu la kufutia familia lilikuwa la wanaume ,jambo ambalo kwa sasa limezikwa kwenye kaburi la sahau.

Baba Levo
Baba Levo
Image: Instagram

Msanii wa Tanzania, Revokatus Kipando, almaarufu Baba Levo, kupitia kituo kimoja cha Radio amefunguka kuhusu ndoa  huku akisema kuwa nyingi yazo huvunjika mwanamke anapopata ajira.

Kulingana na Baba Levo wanawake wengi kwenye ndoa wakipata hela zao hudharau ndoa  kwa misingi kwamba wanaweza kujikimu.

"Asilimia kubwa ya  kuvunjika kwa ndoa  nyingi zinachangiwa na wanawake, wanapota fursa ya kujifanyia kazi wanapopata hela zao wengi huanza kuwadharau wanaume wao kwa kuwa wanaweza kujigharamia kimaisha,"alisema.

Msanii huyu alidokeza kwamba kulingana na tamaduni zilizotumika miaka ya nyuma wanawake hawangeruhusiwa kufanya kazi ,jukumu la kufunya kazi ilikuwa la wanaume ,jambo ambalo kwa sasa limezikwa kwenye kaburi la sahau.

"Ndoa za kitambo zilidumu kwa kuwa mila zingefuatwa ila kwa sasa kuna mashirika yamejitokeza kutetea haki za wanawake ndio chanzo cha wana wanawake kupata fursa ya ajira jambo ambalo limechangia talaka,"alisema.

Baba levo kwenye kauli yake aliongeza kuwa wanawake wengi hawajazoea kujifanyia ajira ila kwa wakati wanapopata ajira wengi zile hela wanazopata huwachanganya zaidi.

"Wanawake wakipata hela wanachanganywa nazo huku wengi wakitaka kuishi maisha yao wenyenye bila usubufu wotote,"alisema Baba Levo.