Msanii wa injili ambaye pia ni mchungaji Size 8 amemmiminia sifa mpenzi wake DJ Mo akisherekehea siku yake ya kuzaliwa.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Size 8 aliandika ujumbe wenye aya ndefu zenye makopa kopa ya mapenzi akimtaja mumewe kama mtu wa kwanza mwenye umuhimu wa hadhi iliyotukuka katika maisha yake.
Size 8 alifichua kwamba kwake, DJ Mo ni kama Abrahamu wa Biblia ambaye anafahamika na Wakristu kama baba wa Imani na busara isiyo na kikomo.
Pia alifichua kwamba anamuita Bwana kwa vile anamuona kama mdosi wake.
“Happy birthdayπ°... Heee hi ni Mali ni safi sana π....... Asante Yesu..... Happy birthday swity @djmokenyaπ. Nakuita Abraham uliyejaa hekima na babe nakuita bwana yani mdosi wangu.....nakupenda sana na waaa am so proud of you swity WEH!” Size 8 alimpetipeti mumewe baba wa watoto wawili.
Mchungaji Size 8 pia aliendelea kumsifia mumewe kwamba kupitia kwa uwezo wa Mungu ameweza kufanikisha mingi huku akimsifia kuwa mwanamume ambaye hashindwi na chochote anachoanza kukifanya.
Size 8 alifichua kwamba mume wake ndiye amekuwa akifanya kazi nyingi nyuma ya pazia ili kufanikisha chapa yake ambayo watu wengi wanaiona baada ya kazi ngumu kukamilika – kazi ngumu ambayo aghalabu hufanywa na DJ Mo.
“Si kwa neema ya Mungu umepata mengi sana! I admire the fact that you don't give up kirahisi na unasonga mbele bila kujali vikwazo.... asante kwa kuwa nyuma ya pazia kwa kweli kusukuma brand na huduma yangu Mungu akubariki...... Wewe ni Baba wa mfano kwa watoto wetu. Tunakutakia siku njema ya kuzaliwa ZAWADI YANGU KUTOKA KWA MUNGU @djmokenya ππβ€οΈ” Pasta Size 8 alimsifia.