logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Dem wa FB afurahi baada ya Mike Sonko kumlipia rent na kumfanyia shopping ya zaidi ya 10k

Dem wa FB amekuwa akifanya kazi na Obinna kwa muda sasa na pamoja wameonekana kufanya kazi ya kupendeza.

image
na Davis Ojiambo

Burudani22 May 2024 - 06:29

Muhtasari


    Dem wa FB azawadiwa na Mike Sonko

    Mchekeshaji na mkuza maudhui chipukizi, Dem wa Facebook ameonyesha furaha yake baada ya mwanasiasa na mhisani Mike Sonko kumlipia kodi ya nyumba ya shilingi elfu 10 na pia kumpa hela ya matumizi.

    Sonko alikuwa katika kipindi cha Obinna Show Live wakati alitambulishwa kwa mrembo huyo ambaye wanafanya kazi bega kwa began a Obinna.

     Sonko alifurahi kumjua na kumpigia mkewe simu kumjulisha kuhusu Dem wa FB kabla ya kumpa simu waongee na yeye.

    Baadae Obinna alimtania Sonko kumlipia Dem wa FB kodi ya nyumba ya kila mwezi, jambo ambalo Sonko alidakia na kumuuliza anaishi kwa nyumba ya gharama gani.

    Dem wa FB alimjulisha Sonko kuwa anaishi katika nyumba ya kodi ya kila mwezi ya 10k, kabla ya Sonko kuzama mfukoni na kuibua mkono na burunguti la noti na kuanza kumhesabia Dem wa FB noti moja baada ya lingine hadi elfu 10.

    Kando na hapo, Sonko pia alimpakulia bunda la noti zisizohesabika Dem wa FB na kumwambia kuwa hizo ni za matumizi yake huku akimtania kutafuta mpenzi wa kumgharamikia katika mahitaji yake mengine.

    “Naeza mlipia kodi ya nyumba kidogo ya huu mwezi, na pocket money kidogo. Halafu utatafuta chali akulipie vitu vingine si ndio,” Sonko alimtania Dem wa FB ambaye alishukuru kisha kuziweka hela zake mfukoni.

    Dem wa FB amekuwa akifanya kazi na Obinna kwa muda sasa na pamoja wameonekana kufanya kazi ya kupendeza katika kukuza maudhui kwenye chaneli ya YouTube.

    Mwezi mmoja uliopita, Obinna aliwarai mashabiki wa kipindi chake kumnunulia Dem wa FB simu, ambapo alikwenda hatua mbele na kumchukulia iphone ya lipa mdogo mdogo na kusema kwamba watakuwa wanailipia kwa hisani ya mashabiki wake.


    RADIO JAMBO FREQUENCIES

    Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


    logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved