Mchungaji T Mwangi amedhihirisha furaha yake baada ya kupokezwa silver button yake kutoka kwa jukwaa la YouTube kwa kufikisha wafuasi laki moja.
Mwangi alifichua taarifa hizi kupitia kurasa zake kwenye mitandao ya kijamii akionesha zawadi hiyo na kushukuru watu wote ambao wamekuwa wakifuatilia mahubiri yake kwenye video zake za YouTube.
Mwangi alisema kwamba ana uhakika wafuasi hao laki moja ni jamii moja kubwa ya Mungu ambayo imekutanishwa kwenye chaneli yake kwa kusudi la kumjua, kumpenda na kumtumikia Mungu.
“Tumefikia watu 100,000 waliojisajili, na nimejawa na shukrani kwa kila mmoja wenu. Safari hii imekuwa ya ajabu, na kwa kweli nimenyenyekezwa na jumuiya ambayo Mungu ameileta pamoja hapa.”
“Asante kwa msaada wako, maombi, na kwa kuniruhusu kushiriki Neno la Mungu pamoja nawe. Iwe ni kwa ibada za kila siku, jumbe za kutia moyo, au nyakati za maombi, kujifunza Biblia, hekima, ni heshima kutembea safari hii ya imani pamoja nawe,” Pastor T alisema.
“Hatua hii muhimu sio tu kuhusu idadi-inahusu maisha yaliyoguswa, mioyo iliyotiwa moyo, na roho zinazosogezwa karibu na Yesu. Ninaamini Mungu ana mambo makuu kwa ajili yetu tunapoendelea kukua pamoja katika imani na makusudi. Hebu tuendelee kuinuana, kueneza upendo Wake, na kuangaza nuru Yake katika yote tunayofanya. Bora zaidi bado kuja!” aliongeza.
Mchungaji huyo wa kanisa la Life Church, Limuru amejizolea umaarufu katika miaka ya hivi karibuni kutokana na upekee katika kutoa maelezo ya Kibiblia kuhusu masuala ibuka kaitka jamii za kisasa.